KATIKA kutoa shukrani kwa Watanzania wote waliowajibika katika kuhakikisha wanamsaidia mwigizaji na mtayarishaji mahiri wa filamu kutoka Swahiliwood Juma Kilowoko ‘Sajuki’ kupatiwa matibabu kutokana na maradhi ya tumbo na kwenda kutibiwa Nchini India na kupona, kampuni ya Wajey Film Company imeandaa tamasha kubwa la shukrani.
Wastara Juma ‘Stara’ amesema kuwa baada ya mumewe Sajuki kupata matibabu anatumia fursa hiyo katika kuwashukru watanzania waliojitoa kwa hali na mali katika kufanikisha matibabu hayo.
“Sisi kama familia hatuna cha kuwalipa watanzania kwa moyo wao wa upendo walioonyesha kwetu, katika kipindi kigumu na majaribu wakati Sajuki akiwa anaugua, si rahisi kumfikia kila mtu kwa wakati mmoja lakini kwa njia ya tamasha hilo tutawafikia, tunawapenda watanzania mungu awabariki sana,”anasema Stara.
Tamasha hilo linatarajia kufanyika leo jumapili tarehe 25/11/2012 katika uwanja wa Samora huku wasanii wa muziki wakitumbuiza kwa nguvu Mzee Yusuf, Linah, H. Baba na mchekeshaji Kitale ataimba burudani kubwa ni pale mechi kali itakapopigwa kati ya wasanii nyota wa filamu kutoka Bongo movie na timu kali ya watangazaji wa redio zote mkoani Iringa.
Ni Tamasha la aina yake kila mwairinga anatakiwa asilikose kwani ni tamasha la kipekee kufanyika Iringa, pia Stara alisema onyesho hilo litafanyika kwa ajili ya kukusanya fedha zitakazopelekwa kwa wasanii wanaosumbuliwa na maradhi na kukosa matibabu alisisitiza mratibu huyo.
Baada ya mechi burudani itahamia ukumbi wa club V.I.P kwa kiingilio cha Tsh 3000 na uwanjani kiingilio ni buku tatu tu
No comments:
Post a Comment