Makubwa Haya;Jengo Lajengwa Mtwara Jiwe La Msingi Lawekwa Dar
Habari ya jumapili ndugu zangu, ni matumaini yangu siku imeanza vyema
ila poleni kwa wote ambao siku ya leo haijanza vizuri kwao ila naamini
itaisha vizuri kwao.
Leo nimewasili majira ya saa mbili mkoani mtwara nikitokea Jijini Dar
kikubwa ambacho nimekiona katika mkoa huu ni mandahari ya kuvutia ya
uwanja wa ndege ambao sehemu kubwa ya jengo la uwanja limekarabatiwa
,sina budi kuwapa sifa mamlaka zinazohusika na viwanha vya ndege kwa
kazi nzuri na ni wito wangu kazi ya ukarabati iendelee na kwa viwanja
vingine pia.
Nikiwa bado nashangaa mjini wa mtwara, niliweza kumuuliza maswali wawili
matatu mwenyeji wangu kuhusu historia ya mkoa huu ukiachilia mbali yale
ninayoyafahamu ambayo nimesoma kwenye Somo la jiografia nikiwa shule.
Swali kubwa lilikuwa kwanini watu wa mikoa ya kusini wamekuwa
wakilalamika kuwa wametengwa na shughuli za kimaendeleo, mfano
miundombinu nk, jibu likikuwa jepesi sana mwenyeji wangu aliniambia
Historia ndio inayofanya mikoa hii kuwa nyuma aliweza kuniambia mengi
kuhusu historia.
Swali hili linipa jibu ambalo sikutegemea kulisikia ila lilinistua na
kunifanya nisahau kuuliza kwa undani je ni historia ipi iliyoitenga
mikoa ya Kusini na maendeleo nikajikuta naama nje ya mada, na kudadadisi
kitu kingine na swali lilikuwa hivi, JE GAS IMEINUFAISHA VIPI MKOA
HUU?, hapa ni kama niliweka chumvi kwenye kidonda kibichi, jibu
lilikuwa gas imekuwa kilio cha wananchi wa eneo ili maana walitegemea
miaka yote waliyosaauliwa katika maendeleo baada ya eneo lao kutumika
uwanja wa mapambano wakati ukombozi kusini mwa bara la africa hasa nchi
za Msumbiji,zimbabwe, labda gas hiyo ingeziba matundu ya simanzi
yaliyopo mioyoni mwao labda gas ingekuwa fidia ya kucheleweshewa fursa
za maendeleo.
Hayo ni maswali ambayo wananchi wa kusini wamekosa majibu ya
kuwaridhisha leo hii wanahoji iweje Rais azindue mradi wa Gas jijini dar
wakati Gas ipo mtwara, ni kufikia kutoa mfano ni sawa jengo linajengwa
Mtwara kisha Jiwe la Msingi linaweka Dar hapa wananchi wanahisi hatua
hii itazidi kuchelewesha maendeleo zaidi katika mkoa wao maana wanahoji
kama gas itakuwa ianpatikana dar je wawekezaji wataona umuhimu gani wa
kuja kuwekeza Mtwara?
Binafsi sipendi kuwa jaji katika jambo hili kuhukumu kama nia ya
serikari ni mbaya au la labda wananchi wanaona wamesalitiwa wanatamani
hiki walichobarikiwa na Mungu kiwatoe katika hali ya umasikini nadhani
hii ni fursa sasa ya serikari kuona ni namna gani wananchi wa maeneo
haya hawapotezi imani na Serikari ya , yapo mambo muhimu serikari
inaweza kufanya ili wananchi hawa wasizidi kusononeka zaidi mi nashauri
kama yawekena hata kama Gas itasafirishwa kwenda popote ila nadhani
wananchi wa maeneo haya wangepewa kipaumbea maana tunaambia Gas
inakwenda kuzalisha umeme hivyo nadhani wananchi wa mikoa ya kusini
wangefikiriwa hata kupunguziwa gharama ya nishati ya umeme kwangu mimi
hii naona itakuwa moja ya jawabu .
No comments:
Post a Comment