Sehemu ya Bandari ya Dar es
Salaam nchini Tanzania ambayo hutumiwa na baadhi ya nchi za Afrika Mashariki
kupokelea bidhaa zao.
 Uchumi katika 
kanda ya Afrika Mashariki uliendelea  kuimarika mwaka uliopita, 2012 
licha ya changamoto lukuki iliyokabiliana  nazo.Kanda nzima ilionyesha 
uchumiwake kukua kwa nguvu na  kusukuma juhudi za kuimarisha mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). 
EAC inajumuisha nchi tano 
wananchama  ikiwa ni pamoja na Kenya,Uganda, Tanzania, Rwanda na 
Burundi, Mwandishi Isaac Mwangi wa Shirika Huru la  Habari la Afrika 
Mashariki (EANA) anaadika zaidi katika Makala haya:
Kwa mujibu wa taarifa rasmi  
zinazotolewa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) kila baada ya miezi 
mitatu,  pato la mwaka katika robo ya kwanza ya mwaka uliopita 
liliongezeka kwa asilimia  7 katika nchi za Rwanda na Tanzania na kiasi 
kikubwa cha kuongezeka kwa pato pia  liliripotiwa nchini Uganda.
Uganda iliripoti pato chanya la 
kukua  kwa uchumi wake katika robo ya kwanza ya mwaka 2012 kufuatia 
kukua kwa hasi kwa  uchumi wake katika robo ya mwisho ya mwaka 2011.
Uchumi wa Burundi kwa upande wake 
 uliendelea kuathirika vibaya kutokana na mambo mbalimbali ikiwa ni 
pamoja na  kuongezeka kwa mfumuko wa bei,kushuka kwa makusanyo ya mapato
 ya serikali na  wabia wa maendeleo kujitoa kuunga mkono juhudi za 
serikali.
Viashiria vya uchumi katika kanda hiyo  ya Afrika Mashariki, vimeonyesha dalili kubwaya
 kukua kwa uchumi  wa kanda hiyo katika robo ya kwanza ya mwaka jana, 
ikiwa ni pamoja na kwenye  sekta za huduma nchini Rwanda na viwanda 
nchini Uganda na Tanzania.
Hali ya kushuka mara kwa mara kwa 
 thamani ya fedha katika kanda hiyo pia ilipungua katika kipindi chote 
cha robo  ya pili ya mwaka 2012 ikiwa ni ishara ya kuwepo kwa sera nzuri
 za fedha  zilizowekwa na mamlaka za udhibiti wa fedha katika kanda.
Viashiria vingine vya kupungua kwa
  mfumuko wa bei ni pamoja na kupungua kwa bei ya mafuta na mavuno 
mazuri ya  vyakula yaliyotokana na hali nzuri ya hewa na kuimarisha 
mikakati ya uzalishaji  kama vile Mpango wa Kuimarisha Mazao nchini 
Rwanda na Kilimo kwanza nchini  Tanzania. 
Pia viwango vya wastani vya  
ubadilishanaji wa fedha za kigeni umepunguza makali ya kuleta mfumuko wa
 bei  miongoni mwa nchi wananchama.
Utafiti uliofanywa na jarida moja la  African Business Magazine
 umebaini kwamba ukuaji endelevu wa  uchumi wa Tanzania unatokana na 
uendeshaji mzuri wa makampuni kwa kufuata sheria  na taratibu na hivyo 
kuongeza idadi ya makampuni ya Kitanzania katika Kundi la  Makampuni 25 
ya Juu Afrika Mashariki kutoka matatu yaliyokuwepo hadi sita katika  
kipindi cha mwaka mmoja tu. 

Kampuni ya Azam ni moja ya vielelezo tosha vya Ukuaji wa Uchumi kwa
Kanda ya Afrika Mashariki hasa nchini Tanzania kutokana na jinsi kampuni hiyo
ya uzalishaji wa Bidhaa mbalimbali za Chakula inavyofanya kazi zake katika Nchi
za Afrika Mashariki 
Kwa upande mwingine uchumi wa 
Kenya  haukukua kwa kasi kama nchi nyingine za Afrika Mashariki na 
badala yake ilipata  ongezeko la ziada la idadi ya watu. Uchumi wa 
Uganda umeongezeka kutokana na  matarajio ya kupata mafuta nchini humo.
Kenya imeripoti kukua kwa uchumi 
wake  kwa kiwango cha chini zaidi cha asilimia 3.5 katika kipindi cha 
miaka minne  iliyopita. Kiwango hicho kinashindana kihafifu na ukuaji 
kwa nchi nyingine za  kanda hiyo. Rwanda asilimia 7.9, Uganda asilimia 
7.2 na Tanzania asilimia 6.7.  Kenya pia amejikuta ikiwa na kiwango 
kikubwa zaidi cha mabadiliko ya mfumuko wa  bei kutoka asilimia 19.7 
Novemba mwaka jana hadi kufikia asilimia 4.1 mwezi huu. 
Ufanisi wa uchumi wa Kenya kwa 
mwaka  huu wa 2013 utapatikana kwa kiasi fulani kutegemeana na jinsi 
gani nchi hiyo  itakavyoendesha uchaguzi wake mkuu mwezi Machi.Kwa kuwa 
ndiyo nchi yenye nguvu  zaidi za kiuchumi katika kanda hiyo,ufanisi wake
 pia utaathiri nchi nyingine  wananchama wa EAC.
Nchini Burundi, mfumuko wake wa 
bei umekuwa  ukishuka mwaka hadi mwaka kutoka asilimia 25.2 mwezi Aprili
 (ikiwa ni kiwango  cha juu zaidi Afrika Mashariki) hadi asilimia 17.3 
mwezi Juni kutokana na  kushuka kwa bei za vyakula. Hatua ya kupungua 
kwa mfumuko wa bei za vyakula  inatokana na juhudi za serikali kuondoa 
kodi za vyakula vya msingi  vinavyoingizwa nchini humo kutoka nje.
Hatua hiyo ambayo ilianza  
kutumika tangu Mei 15, iliishia Desemba 31, mwaka jana. Bidhaa za 
vyakula  zilizohusika kutotozwa kodi ni pamoja na unga wa muhogo, 
mahindi na mtama na  maharage, mchele, viazi,samaki na mafuta ya 
alizeti. Mavuno mazuri ya mazao ya  vyakula pia yamesaidia kupungua kwa 
bei za vyakula.
Licha ya kuongezeka kwa hofu ya 
vitendo  vya ugaidi,sekta ya utalii ilifanya vizuri huku kukiwa na idadi
 kubwa ya hoteli  mpya na maeneo ya kupumzikia yaliyofunguliwa ili 
kuendana na idadi kubwa ya  watalii waliokuwa wanamiminika ndani ya 
kanda hiyo ya EAC.

No comments:
Post a Comment