Friday, August 22, 2014

Ukraine :Msafara wa msaada ni uvamizi


Ukraine inadai kuwa Msafara wa msaada kutoka Urusi ni uvamizi
Maafisa wa Serikali ya Ukraine wmeilaumu serikali ya Urusi kwa kuivamia ardhi ya Ukraine.
Taarifa hiyo imewadia muda mchache tu baada Urusi kutangaza kuwa msafara wa misaada utavuka mpaka na kuingia katika ardhi ya Ukraine bila idhini ya Kiev baada ya kusubiri idhini mpakani kwa zaidi ya juma moja.
Urusi iliamuru msafara huo kuingia Ukraine baada ya Kuilaumu Kiev kwa kuweka vikwazo ilikuzuia msafara huo usiwafikie walengwa .
Valentyn Nalyvaychenko, mkuu wa kitengo cha usalama wa ndani cha SBU amesema kuwa huo ni uvamizi .
Msaada huo umelengwa kuwafaidi wenyeji wa mashariki mwa Ukraine eneo linalokabiliwa na vita .
Taarifa zinasema kuwa msafara huo unapewa ulinzi na wapiganaji wanaotaka kujitenga na Ukraine wanaoungwa mkono na Urusi.
Msaada huo ulikuwa umekwama mpakani kwa juma moja
Shirika la Msalaba mwekundu limekana kuhusika na msafara huo kwa hali yeyote.
Wizara ya maswala ya kigeni ya Urusi imeionya Ukraine isidhubutu kuizuia msafara huo lakini haikusema itachukuwa hatua gani endapo Kiev itazuia msafara huo wa msaada.
Awali Waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi alitangaza kuwa mfasara wa msaadawa Urusi uliokuwa umekwama mpakani sasa umevuka mpaka na kuingia Ukraine.
Aliilaumu Ukraine kwa kuzuia msafara huo mpakani ili kujiingiza kwenye vita dhidi ya waasi wa Urusi eneo la Luhansk.
Katika taarifa aliyotoa ,alisema msafara huo wa msaada wa kibinadamu unaelekea Luhansk.
Mapigano yanaendelea Masharikimwa Ukraine
Wanahabari kwenye mipaka walishuhudia malori yakiingia Ukraine.
Ukraine inahofia msafara huo ni sehemu ya kuingiliwa kati na Urusi Mashariki mwa Ukraine.
Urusi inakanusha madai inawapa silaha na kuwapa mazoezi waasi Luhansk na maeneo yaliyokaribia ya Donetsk ambapo kwa miezi mine vita vimeendelea na kuwaacha zaidi ya watu 2000 wameaga dunia na wengine 330000 kutoroka makwao.
Jiji la Luhanska limezingirwa na waasi na wanajeshi wa serikali na kuwaacha wakaazi bila ya maji,umeme na mawasiliano kwa siku 20

No comments: