Mmoja wa viongozi wa CHADEMA, Singida mjini John Kumalija, akipeana mkono na DC Mpya wa Wilaya Manyoni, Fatuma Toufig |
Singida
Mei 16, 21012.
WAKUU wapya wa Wilaya wanne kati ya watano, waliopangwa kufanya kazi mkoa Singida, jana wameapishwa na mkuu wa Mkoa Dk. Parseko Kone.
Wameapishwa viwanja vya jengo la mkuu Mkoa Singida.
Mkuu wa Wilaya mpya Mkalama, Moshi Chang’a, ameahidi kukabiliana na changamoto zilizopo katika wilaya hiyo kwa kushirikiana na wananchi vyema, kuzikabili changamoto zilizopo.
Amesema anajua wilaya yake mpya nina wakulima hodari na wachapa kazi, hali itakayompa ari ya kushirikiana nao katika kuijenga wilaya hiyo.
Mkuu wa Wilaya Manyoni, Fatuma Toufiq, yeye ameahidi kushughulikia zaidi masuala ya kijamii, hasa kuwainua wanawake, na atafuatilia masuala ya afya na elimu.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya mpya ya Ikungi, Manju Msambya, yeye ameahidi kushughulikia zaidi elimu na kilimo, kutokana na wilaya hiyo kuwa na wakulima wazuri.
Amesema, tatizo la elimu lazima lipatiwe ufumbuzi, kufuatia baadhi ya wanafunzi kuchaguliwa kujiunga sekondari, huku wakiwa hawajui kusoma.
Na mkuu wa wilaya Singida, Queen Mlozi, alisisitiza ushirikiano wa wananchi na viongozo wote, ili kuisogeza wilaya hiyo mbele.
Mkuu mpya wa wilaya kongwe ya Iramba, Yahaya Nawanda hakuwepo katika hafla hiyo, kutokana na kupata udhuru.
Na Elisante John
No comments:
Post a Comment