KLABU BINGWA AFRIKA kujulikana Jumamosi huko Tunis, Esperance v Al Ahly!!
>>BINGWA kuzoa DOLA 1.5 MILIONI!!
>>BINGWA kucheza FIFA KLABU BINGWA DUNIANI Japan Desemba!!!
>>ESPERANCE kuungana na Al Ahly, Mazembe & Enyimba kuwa Klabu PEKEE ZILIZOTETEA VYEMA TAJI LAO??
Mechi ya marudiano ya Fainali ya kutafuta Klabu Bingwa Afrika, CAF CHAMPIONS LIGI, kati ya Mabingwa watetezi Esperance ya Tunisia na Al Ahly ya Misri itachezwa ndani ya Rades Stadium huko Tunis leo hii, Tunisia Jumamosi Oktoba 17 na Timu hizi zinaingia Uwanjani baada ya kutoka 1-1 huko Cairo, Misri huku Esperance wakitaka sare ya 0-0 au ushindi ili kujiunga ile Klabu Spesho ya Timu 3 tu katika historia kuweza kutetea vyema Taji lao la Ubingwa wa Afrika.
Mechi ya marudiano ya Fainali ya kutafuta Klabu Bingwa Afrika, CAF CHAMPIONS LIGI, kati ya Mabingwa watetezi Esperance ya Tunisia na Al Ahly ya Misri itachezwa ndani ya Rades Stadium huko Tunis leo hii, Tunisia Jumamosi Oktoba 17 na Timu hizi zinaingia Uwanjani baada ya kutoka 1-1 huko Cairo, Misri huku Esperance wakitaka sare ya 0-0 au ushindi ili kujiunga ile Klabu Spesho ya Timu 3 tu katika historia kuweza kutetea vyema Taji lao la Ubingwa wa Afrika. Ni Al Ahly, TP Mazembe ya Congo DR na Enyimba ya Nigeria pekee ndio ziliwahi kufanikiwa kutetea vyema Taji la Ubingwa wa Afrika.
Esperance, ambao wametwaa Ubingwa wa Afrika Mwaka 1994 na 2011, wana kibarua kigumu kwani licha ya Al Ahly kuwa Mabingwa wa Afrika mara 6, Klabu hiyo ya Tunisia itaingia kwenye Mechi hii bila ya Nyota wake kadhaa ambao ni majeruhi na wengine wapo kifungoni.
Wachezaji ambao wana Kadi na hawatacheza ni Staa wao kutoka Ghana, Harrison Afful, na Sameh Derbali na majeruhi wao ni pamoja na Majdi Traoui.
Al Ahly itamkosa Beki Sayed Moawad ambae ameumia mguu lakini mmoja wa Makocha wao, Mohamed Youssef, amesema wataziba pengo hilo na wataingia Uwanjani kwa lengo moja tu la kushambulia mwanzo hadi mwisho.
Na ili kudhibiti usalama Uwanjani, Uwanja wa Rades, ambao kawaida huingiza jumla ya Mashabiki 60,000, kwenye Fainali hii ni Watu 35,000 tu ndio wataruhusiwa kuingia. Mshindi wa Fainali hii atatawazwa kuwa Klabu Bingwa Afrika na kuzoa kitita cha Dola Milioni 1 na Nusu na pia ataiwakilisha Afrika katika Mashindano ya FIFA ya kusaka Klabu Bingwa Duniani yatakayochezwa huko Japan Mwezi Desemba.
No comments:
Post a Comment