Saturday, November 17, 2012

ENGLISH PREMIER LEAGUE: ARSENAL 5 vs TOTTENHAM SPURS 0 - ADEBAYOR AFUNGA GOLI NA KUPEWA KADI NYEKUNDU !!


Mchezaji wa zamani wa Arsenal, Emmanuel Adebayor, ambae aliihama Klabu hiyo na kutokomea Manchester City na kisha kuishia Tottenham, leo kwenye Dabi ya London ya Kaskazini,aliiletea Spurs raha pale alipofunga Bao la kwanza katika Dakika ya 10 na Dakika 7 baadae akaishushia Timu yake karaha kubwa alipopewa Kadi Nyekundu kwa rafu mbaya kwa Santi Corzola nakuipa Arsenal mwanya mkubwa kurudisha Bao hilo na kuinyuka Tottenham jumla ya Bao 5-2.

Refa - Howard Webb akiteta na wachezaji wa pande zote mbili baada ya Adebayor kufanya madhambi


Web akitoa kadi nyekundu kwa Adebayor

MAGOLI:
Arsenal 5
Mertesacker 24′ Podolski 42′ Giroud 45′ Cazorla 60′ Walcott 90′
Tottenham 2
Adebayor 10′ Bale 71′
Baada ya Bao la Adebayor na kisha kutolewa kwake, Arsenal ilikuja juu na kufunga Bao 3 kabla Haftaimu kupitia Mertasaker, Podolski na GIrould na Kipindi cha Pili kuongeza nyingine mbili zilizofungwa na Carzola na Walcott. 
Bao la pili la Tottenham lilifungwa na Gareth Bale. Ushindi wa leo umeifanya Arsenal ichupe hadi nafasi ya 6 ikiwa na Pointi 19 kwa Mechi 12. Mertesacker akiifungia timu yake ya Arsenal goli la kwanzaArsenal wakishangilia baada ya Mertesacker kufunga goli la kwanza

Podolski akishangilia baada ya kufunga goli dhidi ya Spurs leo hii

Giroudakishangilia baada baada ya kufunga goli

RATIBA/MATOKEO:
Jumamosi, Novemba 17, 2012
Arsenal 5 Tottenham Hotspur 2
[SAA 12 Jioni]
Liverpool v Wigan Athletic
Manchester City v Aston Villa
Newcastle United v Swansea City
Queens Park Rangers v Southampton
Reading v Everton
West Bromwich Albion v Chelsea
[SAA 2 na Nusu Usiku]
Norwich City v Manchester United


MSIMAMO TIMU ZA JUU

1 Man United Mechi 11 Pointi 27
2 Man City Mechi 11 Pointi 25
3 Chelsea Mechi 11 Pointi 24
4 Everton Mechi 11 Pointi 20
5 WBA Mechi 11 Pointi 20
6 Arsenal Mechi 12 Pointi 19
7 West Ham Mechi 11 Pointi 18
8 Tottenham Mechi 12 17


VIKOSI:
Arsenal: Szczesny, Sagna, Mertesacker, Koscielny, Vermaelen, Wilshere, Arteta, Cazorla, Walcott, Giroud, Podolski
Akiba: Mannone, Andre Santos, Oxlade-Chamberlain, Ramsey, Coquelin, Arshavin, Jenkinson.
Tottenham: Lloris, Walker, Gallas, Vertonghen, Naughton, Lennon, Sandro, Huddlestone, Bale, Adebayor, Defoe
Akiba: Friedel, Dempsey, Dawson, Sigurdsson, Livermore, Townsend, Carroll.
Refa: Howard Webb

No comments: