Mtoto Juliana Mwinuka
Majeraha
yaliyotokana na kuungua moto klatika uso wa mtoto mtoto Juliana
Mwinuka (16) mkazi wa kitongoji cha Ushindi kata ya
Mavanga wilaya ya Ludewa mkoa wa Njombe yameanza kuziba taratibu
huku akiwa amefanyiwa oparesheni zaidi ya wiki mbili sasa katika Hospitali ya CCBRT.
Kwa sasa anaendelea vizuri na sura yake imeanza kurudia katika hali ya kawaida japo bado kufanyiwa oparesheni nyingine .
Mtandao huu unaendelea kuwapongeza wote wanaoendelea kuguswa na kuungana na wadau wengine kumchangia fedha za matibabu ,mtoto Juliana kama anavyoonekana akiwa ameunga uso wake kwa moto ni yatima anahitaji msaada wako ili kunusuru maisha yake waweza kutuma mchango wako kwa njia ya M-PESA katika namba hii 0754 026 299 au Tigo Pesa 0712 750199 namba hizi ni za mmiliki wa mtandao huu Bw Francis Godwin
Nawaomba tuungane kufanikisha kuokoa maisha ya mtoto Juliana Mwinuka na Mungu atatuongezea zaidi
No comments:
Post a Comment