Tukio hilo limetokea eneo la Mwangata mjini Iringa na kupelekea polisi kufika kuwatawanya wananchi hao na kuwasaka wale ambao wanadaiwa kueneza uvumi huo.
Hata hivyo hakuna mwananchi hata mmoja kati ya waliokuwepo hapo ambaye amethibitisha kuona msukule huyo zaidi ya kila mmoja kusema amesikia .
Wananchi hao wameizunguka moja kati ya nyumba eneo hilo wakitaka kuichoma moto kwa madai kuwa ndani kuna msukule huyo.
Rai ya mtandao huu kwa jamii ya mkoa wa Iringa na Tanzania kwa ujumla kuepuka kuamini imani za kishirikina ambazo zinaweza kuvuruga amani yetu
No comments:
Post a Comment