Saturday, August 23, 2014

TUNATANGAZA UTALII WA NDANI: FAHAMU HIFADHI YA TAIFA YA ZIWA MANYARA



Ndege wakiwa katika Hifadhi ya Taifa ya Manyara
 Baadhi ya Nyani  wakiwa katika Hifadhi ya Taifa ya Manyara



Tembo wakiwa katika Hifadhi ya Taifa ya Manyara

Picha zote na Francis Godwin

Hifadhi ya Ziwa Manyara ni maarufu sana nchini Tanzania kwa simba wanaopanda miti. aina hii ya simba hupatikanandani ya hifadhi hii pekee barani Afrika. Umaarufu wa hifadhi Ziwa manyara unaongezeka kila siku kutokana na kukua kwa utaliiwa ndani ambapo wananchi wengi kutoka katika mikoa ya kaskazini mwa Tanzania hupenda kutembelea hifadhi hii.
  • Hifadhi hii ipo ndani ya Bonde la Ufa ambalo kingo zake zinaongeza mandhari zaidi. Ziwa Manyara lililo ndani ya hifadhi ni kivutio kikubwa kwa watalii kutokana na wingi wa ndege aina yakorongo walio na mvuto mkubwa kwa kila mtu. Ndege hao huonekana kama pazia kubwa jeupe nyakati za mchana wanapokuwa ziwani kujipatia chakula na mapumziko.
  • Vilevile , umaarufu wa hifadhi ya Ziwa Manyara unakua kutokana na wingi wa wageni wanaotoka nje ya nchi. Idadi kubwa ya wanafunzi kutoka shule mbalimbali nchini Tanzania hutembelea hifadhi hii kujionea maajabu ya dunia hasa viumbe wa porini, wanyama, mimea na ndege.
  • Wanyama wanaopatikana ndani ya hifadhi hii ni pamoja na simba, nyati, tembo, nyani, chui, pundamilia na wanyama wengine wanaokula majani. hifadhi hii pia inasifika kwa wingi wa wake wa ndege hasa heroe na mnandi ambao huonekana katika makundi makubwa na kufanya eneo hili la utalii kuwa na aina 400 za ndege wanaovutia.

  • Mji mdogo wa Mto-wa-Mbu ni kituo kikubwa cha biashara kinachotoa huduma kwa wageni wanaotembelea hifadhi ya Ziwa Manyara.Mji huu mdogo upo karibu na lango la hifadhi.Chemchem za maji moto ni maajabu mengine ndani ya hifadhi hii. Maji hayo yanayobubujika kutoka ardhini huonekana yakitoa moshi kama vile maji yanayochemka jikoni. Chemchem hizi za maji moto ya asili zimekuwa zikibubujika bila kukauka kwa kipindi cha mamilioni ya miaka.
Hifadhi hii iko umbali wa kilometa 126 kutoka Arusha mjini ina ukubwa wa kilometa za mraba 330.

No comments: