Tuesday, April 10, 2012

NAIBU SPIKA JOB NDUGAI AFURAHISHWA NA TAMASHA LA PASAKA DODOMA

Mgeni rasmi wa Tamasha la Pasaka Mkoani Dodoma Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Job Ndugai akipokea CD kutoka kwa Mkurugenzi wa Msama Promotion Alex Msama, inayoitwa "Utukufu Kwa Mungu"ya muziki wa injiili kutoka kwa  Mwanamuziki Solomon Mukubwa wa DRC Congo,  iliyozinduliwa jana kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam na Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernald Membe
Tamasha lingine kubwa limefanyika leo kwenye uwanja wa Jamhuti mjini Dodoma likishirikisha waimbaji lukuki kutoka hapa nchini na nje ya nchi kufuatia lile la jana kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam ambapo mwimbaji wa Afrika ya Kusini Rebecca Malope alitumuiza.
 Mkuu wa Mkoa  waa Dodoma Dk. Rehema Nchimbi akipokea CD yake ya Utukufu kwa Mungu kutoka kwa Mkurugenzi wa Msama Promotion Alex Msama.
 Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Betty Mkwasa akipokea CD yake ya Utukufu kwa Mungu kutoka kwa Mkurugenzi wa Msama Promotion Alex Msama.
 Mgeni rasmi wa Tamasha la Pasaka Mkoani Dodoma Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Job Ndugai akizungumza katika tamasha hilo leo jioni kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. Rehema Nchimbi na kushoto ni Mkurugenzi wa Msama Promotion Alex Msama
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. Rehema Nchimbi na kushoto akiongea na wanadodoma kwenye tamasha hilo ambapo aliwahimiza wananchi wa Dodoma kuufanya mkoa wa Dodoma kuwa makao makuu ya amani nchini, Kushoto ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Job Nduga na katikati ni Alex Msama. 
 
 
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Job Nduga akiongoza viongozi wenzake kucheza muziki jukwaani kushoto ni MC wa Tamasha hilo Charles Mwakipesile.
Mkurugenzi wa Msama Promotion Alex Msama kulia akimuaongoza Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Job Ndugakuelekea jukwaani, kwa ajili ya kuzungumza na mashabiki wa muziki wa injili, kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Betty Mkwasa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. Rehema Nchimbi.
 Kikundi cha nyimbo za injili Nyati kutoka mkoani Dodoma kikitumbuiza
 Mwimbaji Emi Kosgei kutoka nchini Kenya akishirikiana na kundi la mwanamuziki mwenzake kutoka Kenya Anastazia Mukabwa.
 Mwimbaji Emi Kosgei kutoka nchini Kenya akifanya vitu vyake jukwaani kama anavyoonekana pichani.
 Mwimbaji wa Tanzania Kutoka mkoani Dodoma Rose Muhando akishabulia jukwaa pamoja na kundi lake la Kitimtim kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma jioni ya leo.
 Mmoja wa wacheza shoo waliowahi kufanya kazi ya muziki na Rose Muhando akifanya vitu vyake jukwaani huku mwanamuziki huyo akimuangalia kwa furaha.
 Mwanamuziki wa nyimbo za Injili Rose Muhando akiimbisha mashabiki wake mkoani Dodoma kwenye uwanja wa Jamhuri jioni ya leo ambapo tamasha la Pasaka limerindima katika uwanja huo.
 Mwimbaji Upendo Kirahiro naye amefanya mambo makubwa sana jukwaani na kuwafanya mashabiki kumshagilia kwa nguvu.
 Upendo Kirahiro akifanya vitu vyake akishirikiana na waimbaji wenzake jukwaani.

No comments: