NA MWANDISHI WETU
RAIS Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Warsha ya siku moja itakayojadili ukuwaji wa uchumi na changamoto zake, itakayofanyika Mei 24 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Akizungmza leo na wandishi wa habari, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii Nchini (ESRF), Dk. Bohela Lunogelo alisema wameandaa warsha ambayo inatarajiwa kuwakutanisha wadau ambao watachangia mada mbalimbali.
Alisema mada zitakazo jadiliwa siku hiyo zimegawanyika katika sehemu kuu tatu ambapo zote zinahusiana na tafiti mbalimbli zilizofanyika kwa lengo la kuimarisha ukuaji uchumi katika jamii.
Dk. Lunogelo alisema ukiachilia mbali Rais pia atakuwepo Profesa Benno Ndulu ambaye Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania na Dk. Huang Chengwei ambaye ni mtaalamu anashughulika na kuondoa umasikini nchini China.
Alisema kuwepo kwa Dk. Chengwei kutasaidia Watanzania kufahamu mambo mengi ambayo Wachina wameyapitia hadi kupata mafanikio katika uchumi.
Adha, alisema mambo ya takayojadiliwa na wataalamu siku hiyo yatakuwa ni pamoja na madini ukuaji wa viwanda na utalii maswala ya usimamizi wa ardhi na ukuaji wa kilimo.
Mengine ni kuhusiana uongozi, utawala bora na maswala ya miundombinu na uendeleza wa rasilimali na mengineyo.
No comments:
Post a Comment