Saturday, June 9, 2012

AJARI ILIYOTOKEA NDANI YA MANISPAA YA BUKOBA USIKU WA KUAMUKIA LEO

 Gari lilivyoingia ndani ya hotel.








Ni gari aina ya NOAH usiku wa kuamukia leo  imepata ajari ya kutisha sana mara baada ya mmiliki wa gari hilo ambaye nimebahatika kumjua kwa jina moja tu EGDI kushindwa kuliongoza na hatimaye kwenda kugonga nyumba iliyokuwa mbele yake inayotumika kama hotel.
Nikiongea na mmiliki wa hotel hiyo anaseme kuwa majira ya saa nane usiku akiwa amelala na familia yake alisitushwa na mshindo mkubwa kwenye nyumba yake jambo ambalo lilipelekea yeye kudhani kuwa kuna wezi wamevamia nyumba yake ila mara baada ya kuamuka alishangaa kuona gari limepaki katikati ya nyumba yake huku nyumba yake ikiwa imebomoka vibaya.
Chanzo cha habari hakijajulikana mpaka sasa hivi ili mmiliki wa gari hilo amelazwa katika hospitali ya mkoa Kagera kwa matibabu.

No comments: