Mbunge wa Jimbo la Muhambwe Mkoani Kigoma Bw. Felix Mkosamali
amevamiwa na kupigwa na watu anaodai huenda wakawa wapinzani wake
Kisiasa
Tukio hilo dhidi ya Bw. Mkosamali limetokea Jumapili ya wiki iliyopita
juni 3 mwaka huu, majira ya saa 11jioni wakati akitoka katika Kijiji cha
Kumsenga na kagezi kwenda Kibondo mjini
Mbunge huyo amesema akiwa na baadhi ya wafuasi wake katika Siasa,
kabla ya kushambuliwa na kundi kubwa la Vijana walisimamisha Gari
alilokuwa akitembelea ambapo aliteremka akidhani anasalimiana na
wananchi wenye nia njema
Jeshi la Polisi wilayani Kibondo limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na
kwamba linaendelea na uchunguzi zaidi.
No comments:
Post a Comment