SHULE ya Sekondari ya Peace iliyoko Kata ya Kagondo, Manispaa ya Bukoba, inayomilikiwa na Meya wa manispaa hiyo, Anatory Amani, imeingia katika kashfa nzito ya kuwatapeli wanafunzi 84 wa kidato cha nne mwaka 2011.
Amani ambaye pia ni diwani wa kata hiyo, anadaiwa kuwahadaa wanafunzi hao na kisha kuwahamishia shule nyingine ya Bernard ya wilayani Karagwe kwenda kufanya mitihani yao ya mwisho kwa siri na kinyume cha sheria.
Kutokana na udanganyifu huo, Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limeyafuta matokeo ya wanafunzi hao kwa kile kilichoelezwa kuwa majibu yao yalikuwa na ufanano.
Uchunguzi wa Tanzania Daima ulibaini kuwa meya huyo alifanya ujanja huo pasipo kuwashirikisha wazazi wa wanafunzi hao wala kufuata taratibu za uhamisho wa Idara ya Elimu Mkoa wa Kagera.
Wazazi hao walidokezwa kuwa meya huyo amekuwa akiwachuja wanafunzi wa kidato cha nne muda mfupi kabla ya mitihani ya mwisho na kubakiza wale wenye uwezo mkubwa kimasomo ili shule yake ionekane inafaulisha zaidi, hivyo kuwavutia wazazi.
Katika mahojiano na gazeti hili mjini Bukoba, baadhi ya wazazi hao walieleza jinsi walivyopokea taarifa hizo kwa mshangao na masikitiko makubwa na pia kusononeshwa na hatua ya meya huyo kukwepa kukutana nao.
Huku wakionesha orodha ya majina ya wanafunzi hao ambayo Tanzania Daima ina nakala yake, walidai kuwa walilipa ada tangu kidato cha kwanza hadi cha nne.
“Sisi tulishangazwa na hatua ya kutuambia kuwa tunapaswa kuchangia gharama za watoto wetu kwenda Karagwe kufanya mtihani wao wa mwisho katika sekondari ya Bernard, ikiwa ni siku moja kabla ya usajili kufungwa,” walidai.
Mmoja wa wazazi hao, Fredson Rwegasira, ambaye ni mfanyabiashara katika soko kuu la mjini Bukoba, alisema kuwa walipohoji ni kwanini watoto wao wanahamishiwa Karagwe, walijibiwa kuwa hawakufikisha alama za ufaulu na hivyo hawawezi kuendelea kubaki Sekondari ya Peace.
“Unajua meya anamiliki shule mbili hapa Bukoba ambazo ni Aman English Medium Primary na Peace Sekondari, sisi wengine watoto wetu wamesoma kwake toka chekechea, sasa iweje mwanafunzi afikie kidato cha nne ndipo aambiwe hakufikisha alama za ufaulu?” alihoji Rwegasira.
Wazazi hao ambao wengi wao walionekana kuzungumza kwa jazba wakidai watoto wao wameathiriwa kisaikolojia, walimlalamikia meya huyo wakidai anawadharau na kuwapiga chenga.
Walibainisha kuwa walilazimishwa kuchangia sh 180,000 za kuwapeleka Karagwe pamoja na kununua sare za shule ya Bernard, kama kituo cha mitihani, lakini baada ya majibu kutoka, majina yao hayakuwa na matokeo.
“Jamani tumelipa sh milioni 1.5 kila mwaka ambayo hulipwa kwa awamu tatu pamoja na sh 270,000 za masomo ya ziada, halafu leo unasikia mwanafunzi kafutiwa mtihani,” alisema mzazi mmoja.
Kwamba hatua hiyo iliwalazimu kumfuata Ofisa Elimu wa Mkoa wa Kagera, ambaye aliwaeleza kuwa watoto wao wamefutiwa matokeo, hivyo hawaruhusiwi tena kufanya mitihani hadi baada ya miaka mitatu.
“Baada ya kumlalamikia ofisa elimu na kumweleza kilichotokea, naye alishangaa maana hakuwa na taarifa za kuhamishwa kwa wanafunzi wetu kutoka Peace kwenda Bernard,” walisema wazazi hao.
“Sisi tunahoji kama wanafunzi hawa wanarudia mtihani, nani atagharamia maana mwenye shule tulikowakabidhi anatukimbia, kututisha, serikali imekaa kimya, tufanyeje?” alihoji mzazi mwingine.
Alipotafutwa Ofisa Elimu wa Mkoa wa Kagera, Florian Kimoro, kutaka kujua hatua zilizochukuliwa na ofisi yake dhidi ya mmiliki wa Shule ya Peace, alionekana kukwepa.
“Siwezi kutoa ufafanuzi kwa mtu nisiyemuona, njoo ofisini kwangu utapata ufafanuzi,” alijibu Kimoro na kukata simu yake ya kiganjani.
Hata hivyo baadaye alijibu kwa njia ya ujumbe mfupi akisema: “Taarifa hizo sijazipata naomba uwasiliane na Ofisa Elimu wa manispaa kabla ya kuja kwangu.
Meya Aman alipotafutwa alitoa majibu yenye utata ambapo licha ya awali kukiri kumiliki shule hizo, baada ya kubanwa aligeuka na kukana kuwa hana shule anayoimiliki nchini, huku akimlazimisha mwandishi aende ofisini kwake apewe vielelezo.
Mwandishi alifika ofisini kwa meya mara mbili kama alivyotakiwa, ofisi ilikuwa imefungwa muda wote na hata alipopigiwa simu na kutumiwa ujumbe mfupi, hakujibu hadi leo.
Chanzo na www.freemedia.co.tz

No comments:
Post a Comment