Saturday, August 11, 2012

Rais Wa Ghana Anazikwa Leo.

Rais wa Ghana aliyefariki ghafla Marehemu John Atta Mills anazikwa leo kwenye makazi yake katika kasri la Osu.
Viongozi 16 kutoka mataifa mbalimbali barani Afrika miongoni mwao akiwepo pia Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Bibi Hillary Clinton wanatarajiwa kushiriki mazishi hayo.
Marehemu Mills aliyeongoza taifa hilo la Afrika ya Magharibi linalosifika kwa demokrasia zaidi kwenye eneo hilo, alifariki dunia terehe 24 mwezi Julai mwaka huu kwa ugonjwa unaoaminika kuwa saratani ya koo.

No comments: