Saturday, May 11, 2013

DAVID MOYES: SIKUPANGA KUONDOKA EVERTON NA SIKUJUA KAMA SIR ALEX FERGUSON ATASTAAFU GHAFLA NAMNA HII!!!!, OFA HII NILIYOPEWA NI HESHIMA TUPU NISINGELIWEZA KUIKATAA!.


DAVID MOYES amekiri hakuwa anajua kama Sir Alex Ferguson atastaafu Manchester United na yeye kuteuliwa kuwa Meneja huko lakini alipopewa ofa hakusita hata Sekunde moja.

Moyes amesema hatua hii ni kama ile alipotoka Preston North End Mwaka 2002 na kutua Everton.
Ametamka: “Nasikitika kuondoka Klabu safi kama Everton ambayo imekuwa sehemu ya maisha yangu lakini ukweli siwezi kuikataa ofa ya Man United!” 
Ingawa Mkataba wake na Everton ulikuwa ukimalizika Juni 30, David Moyes alithibitisha hakuwa na mipango ya kuhama na alikuwa tayari yeye na Mwenyekiti wa Everton, Bill Kenwright, walikuwa wameshaandaa mipango ya Msimu ujao.
Moyes pia alimzungumzia Mtu atakaemrithi, Sir Alex Ferguson, na kutamka: “Hakuna Mtu aliefikiria ipo Siku Sir Alex Ferguson atastaafu. Tulidhani yeye ni Binadamu wa ajabu. Yeye ni mfano kwa kila Mtu. Heshima yangu kwake haielezeki. Tumetoka zama tofauti. Nimekua nikimwona yeye na Jock Stein ni Mashujaa, baadae nikashindana na Sir Alex. Sina neno lolote ala kumwelezea ambalo litamtendea haki Sir Alex Ferguson!’

Kocha wa muda David Moyes akiwa na wachezaji wa Everton leo kwenye mazoezi ambapo wanatarajia kucheza na West Ham hapo jumapili saa 11 jioni kwenye masaa ya africa mashariki.

Kama kawaida yake umakini na kazi

Kocha mtarajiwa wa United David Moyes akimaliza mechi ya jumapili na West Ham atakaribishwa na Chelsea kwenye uwanja wao Darajani kumaliza msimu huu mchezo utakaochezwa kwa pamoja viwanja 10 saa 12:00 jioni.

Pia Moyes alizungumzia Mechi yake ya mwisho akiwa Meneja wa Everton Uwanja wa Nyumbani Goodison Park ambako Jumapili hii watacheza na Newcastle na kusema anatumaini Mashabiki watatoa heshima kama ile ya Siku ya kwanza yeye kutua hapo.

Kocha wa Everton David Moyes wakati anaojiwa na waandishi wa habari kuhusu mtanange wa jumapili na West Ham

Mechi ya mwisho kabisa kwa David Moyes akiwa Meneja wa Everton ni hapo Mei 19 watakapocheza ugenini Stamford Bridge na Chelsea.

BARCLAYS PREMIER LEAGUE
RATIBA

Jumamosi Mei 11
[Saa 8:45 Mchana]
Aston Villa v Chelsea

Jumapili Mei 12
[Saa 9:30 Mchana]
Stoke v Tottenham
[Saa 11:00 Jioni]
Everton v West Ham
Fulham v Liverpool
Norwich v West Brom
QPR v Newcastle
Sunderland v Southampton
[Saa 12:00 Jioni]
Man United v Swansea

Jumanne Mei 14
[Saa 3:45 Usiku]
Arsenal v Wigan
[Saa 4 Usiku]
Reading v Man City

MECHI ZA MWISHO ZA LIGI MSIMU HUU 

Jumapili 19 Mei
[Saa 12:00 Jioni]
Chelsea v Everton
Liverpool v QPR
Man City v Norwich
Newcastle v Arsenal
Southampton v Stoke
Swansea v Fulham
Tottenham v Sunderland
West Brom v Man United
West Ham v Reading
Wigan v Aston Villa

No comments: