Sunday, June 3, 2012

KATIKA MITANDAO YA KIJAMII

 Ni baadhi ya mawazo ya wadau wangu juu ya Vita vya kagera 
- Wakuu JF heshima mbele sana, naomba kuuliza tena hivi kulikuwa ana ulazima wa kupiagana Vita na Idd Amin mpaka kumuondoa kwenye madaraka nchini mwake? Yeye alivunja sheria za kimataifa kwa kutuingilia ndani ya mipaka yetu, je na sisi kwa kuvuka mipaka yake pia mbona kama tulijivua nguo kama yeye, yaani tukawa two wrongs!

- I mean kumuondoa tu kwenye ardhi yetu ndio sheria za kimataifa zinavyosema, lakini kwenda mpaka kumuondoa kwenye uongozi wa Taifa lake mbona kama we went too far, na historia ikaishia kutusuta maana tukamuweka Obote, akaishia kuondolewa tena na mwingine, au Great Thinkers mnasema je?

- Na wale mabingwa wa Conspiracy Theories karibuni sana!!


William,
Mimi sijui ukweli juu ya vita hii. Ila umenikumbusha kitu ambacho kimenifanya nicheke, ngoja nikushirikishe. Baba yangu alinisimulia wakati wa vita hivyo, (Sikumbuki vizuri maana ni marehemu kwa sasa) alinitajia jina la mtu kama hili lako la pili (Malecera) au Kawawa, alienda kuwatembelea na akaitisha mkutano akawa anawahimiza na kuwatia moyo, "Piganeni wala msiogope chochote". Ghafla ikakatiza ndege ya kivita ya Uganda, alikimbilia kwenye handaki mara moja. Baada ya hapo aliondoka kabisa eneo lile. Kwa maana hii, ule mkutano haujafungwa mpaka kesho, maana alikatisha mara moja.
Lakini pia kama kuna agenda ya siri alikuwa nayo kiongozi wa nchi wakati huo, kama ulivyohisiwa kwamba ndilo lengo la maada yako, basi hakuwa peke yake, waulizeni hata akina Malecera na wengine waliokuwepo wakati huo, nini kilisababisha waingize wazee wetu vitani
.

Quote By chama View Post
Nenda Bukoba ukaseme upuuzi huu wao watakueleza vizuri kwani mpaka leo kovu la vita alilotuletea Idd Amin bado wanalo.

Chama

Gongo la Mboto DSM
upuuzi hapo ni upi mkuu hebu ni dadavulie kidogo basi.Hapa tupo kwa ajiri ya kuelimishana?

Na swala la kovu bukoba siyo ishu kubwa sana ishu hapa ni je tanzania tulikuwa tunaulazima wakupigana ile vita mpaka kuingia nchini uganda??


Ukweli ni kwamba idd amin alikuwa na haki ya kututandika.

Mkuu umbea wa nyerere na kiherehere chake ndo kilicho tuponza.
By LEGE
mkuu unajua kati ya uganda na tanzania ni nani alikuwa mchokozi??

Je? Wajua ni kwanin? Uganda waliitandika tanzania na mpaka kuvuka mipaka??


In short.Nyerere alikuwa swaiba ake sana obote na pind idd amin alipo mpindua abote nyerere hakufurahia kabisa.Hivyo tanzania ilimuhifanyi obote na mkakati kabambe wa kumng'oa idd amin madarakan uliundwa kuna vijana waganda na watanzania walipewa mafunzo na kuanza kumletea choko choko idd amin kwa kuingia uganda na kufanya fujo walivyo fukuzwa walikimbilia tanzania choko choko zikazid wakaenda tena kufanya fujo na wakafanya uharibifu mkubwa sana uganda idd amin akakasirika akawatandika na kuwafukuza mpaka tanzania na kuingia kilomita kazaa tanzania.

Hapo ndipo nyerere alipokuwa anapataka haraka haraka akautangazia umma kwamba idd amin anataka kuitwa baadhi ya ardhi ya tz na kutangaza vita.
Je? Hapo mwenye kosa nani?? Na je? Ni nani hapo ni mchokozi wa mwenzake?

Ndio mana hata kamanda gadafi alimuunga mkono idd amin na kumsaidia kwa sababu uhuni wote alikuwa anaufahamu.
Nenda Bukoba ukaseme upuuzi huu wao watakueleza vizuri kwani mpaka leo kovu la vita alilotuletea Idd Amin bado wanalo.

Chama

Gongo la Mboto DSM

No comments: