BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA) limeonesha kuridhiswa na maendeleo ya shindano la Bongo Star Starch huku likiwataka washiriki wanaopatikana kupitia shindano hilo kujiendeleza wenyewe badala ya kutegemea kusaidiwa na mradi huo pindi shindano linapokwisha.
Wito huo ulitolewa jana na mratibu wa BSS katika Basata Vicky Temu wakati akichangia mada katika mkutano uliowashirikisha BSS na wadau wa sanaa na kufanyika Basata.
Vicky alisema kuwa wasanii hao wanatakiwa kutambua kuwa uhusiano kati ya BSS na wasanii hao unamalizika mara baada ya shindano hivyo wanatakiwa kutumia vema elimu ya muziki waliyoipata wakiwa ndani ya shindano hilo kujiendeleza zaidi.
Hata hivyo alimtaka mwandaaji wa shindano hilo Ritha Paulsen kuwaendeleza wasanii hao ikiwa pamoja na kuingia mkataba na studio za kurekodia muziki kwa lengo la kuwaendeleza zaidi watakaofanya vema pindi shindano linapomalizika.
Wakati huo huo mwandaaji wa shindano hilo Rita, aliwataka waandishi pamoja na watangazaji wa redio na luninga kuwasaidia wasanii watokao katika BSS badala ya kuwakatisha tama.
Alisema kuwa kuna wadau mbalimbali katika vyombo vya habari na sanaa kiujumla ambapo wanawakatisha tamaa wasanii watokanao na mradi wa BSS kwa kutotaka kuwasaidia kuwatangaza.
No comments:
Post a Comment