Friday, May 4, 2012

KUTOA NI MOYO, MSAIDIE NDUGU YETU SAJUKI

Watanzania tumekuwa na kasumba ya kusubili mtu afe ndo tunakuja kuchanga ela kwa ajiri ya mazishi hapa tubadilike ili kukwepa gharama nyingi za mazishi nasungumzia milioni 52 na nyingine kupitia kwenye mitandao.Mwenzetu ni mwigizaji kama Kanumba naye ametuburudisha kwa mda mrefu leo hii anaumwa sana na anahitaji kiasi cha shilingi milion 25 ili akapate matibabu yake nchi india kwa pamoja tusahidiane ili kuweza kuokoa maisha yake.

Je wale waliotoa kwa Kanumba nazungumzia viongozi na vigogo hawana taarifa hizi????????

Je mbona siku ya mazishi ya Kanumba magari yalipangana(foleni) lakini kwa Sajuki hata bajaji hamna wakati kipaji ni kile kile na kuburudisha ni kulekule??????

 
Ndugu zangu Watanzania popote mlipo ulimwenguni tunaombwa kuisaidia familia hii kwa hali na mali kwa jinsi Mungu atakavyotubariki ili waweze kujikimu na maisha yao ya kila siku ikiwa ni pamoja na kupata pesa za matibabu ya Sajuki yanayotarajiwa kugharimu kiasi cha shilingi milioni 25 za kitanzania.

Kama utaguswa kwa namna yoyote ile unaombwa kutuma mchango wako kupia akauti ya benki ya Wastara au kwa m-pesa kwa namba nitakazozitaja hapa chini.

AKIBA COMMERCIAL BANK, ACC NO. 050000003047, WASTARA JUMA
AU
KWA M-PESA NO. 0762 189592

Asanteni sana kwa ushirikiano wenu Mungu awabariki na azidishe kila mtakapopunguza.

No comments: