Thursday, May 3, 2012

Waziri Magufuli Ataka Mkandarasi Kujenga Barabara Usiku Na Mchana

Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akitoa ufafanuzi wa mradi wa mabasi yaendao mwendo kasi (DART) mei 2,2012 jijini Dar es Salaam kwa waandishi wa habari hawapo pichani alipotembelea na kuangalia maendeleo ya  mradi huo ambao utagharimu shilingi bilioni 288 za kitanzania ambazo zitajumlisha kwa pamoja na ujenzi wa vituo vya mabasi. (picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO),

Waziri wa Ujenzi Dr, John Magufuli (mwenye koti jeusi) akikagua upanuzi wa barabara ya Mwenge- Tegeta leo jijini Dar es Salaam. (mwanamke ni )  Kaimu Mkuu wa Mkoa  wa DSM Mwantumu Mahiza,na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi Hebert Mrango (mwenyetai) Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO.
Mkurugenzi Mtendaji wa TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale akitoa maelezo ya mradi wa DART  Mei 2,2012  jijini Dar es Dar es salam kwa Waziri wa Uchukuzi  Dkt. John Magufuli (wapili kushoto)  pamoja na  Kaimu Mkuu wa Mkoa wa DSM Mwantumu Mahiza, (kushoto). Mradi huo ukikamilika utasaidia kupunguza msongamano wa  magari na kurahisisha usafiri kwa wakazi wa jijijni. (Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO).

Baadhi ya sehemu ya ujenzi wa daraja huko mbezi- (mwenge- Tegeta
NA  MAGRETH KINABO – MAELEZO

 WAZIRI wa  Ujenzi , Dk. John Magufuli amemtaka mkandarasi wa ujenzi  wa Barabara ya  Mabasi yaendayo kasi(DART) yenye urefu wa kilomita 21 na vituo vya mabasi 29 kutoka Kimara hadi Kivukoni iliyoko Jijini Dares Salaam kufanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha
Kauli hiyo imetolewa  na Waziri Magufuli leo wakati alipotembelea miradi hiyo miwili  ili  kungalia shughuli za ujenzi  ambapo alifurahishwa na kazi hizo huku akiwataka wamalize kwa muda unaotakiwa.
“Mkandarasi unatakiwa kufanya kazi usiku na mchana ili kazi ikamilike kabla ya wakati kampuni yenu ni kubwa kama kuna matatizo yoyote mtuambie sisi serikali ili tuweze kuyashughulikia,” alisema Waziri Magufuli.
Waziri Magufuli pia ametoa muda wa siku saba kwa Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania(TANESCO) na  Mamlaka ya  (DAWASA) kuondoa miundombinu yao haraka ili kuepusha ucheleweshaji wa mradi  wa DART.
Waziri wa Magufuli alitembelea ujenzi huo katika maeneo ya Jangwani na Ubungo, ambapo alisema itagaharimu sh. bilioni 240 na ikijumwuishwa na ujenzi  mwingine wa vituo utagharimu jumla ya bilioni 288 ambazo zimetolewa na Serikali na Benki ya Dunia.
Awali Meneja wa mradi , Frank  Rohde kutoka  kampuni hiyo ,  alisema changamoto inayoukumba mradi huo ni ucheleweshaji wa vifaa vya ujenzi huo kutoka bandarini ambapo vimekaa kwa muda wa siku saba.
Akizungumzia kuhusu  tatizo hilo Waziri Magufuli alisema atazungumza na Wizara ya Fedha na Mamlaka ya Mapato(TRA) ili vifaa hivyo vitolewe haraka.
Aidha Waziri Magufuli amemtaka Mkandarasi na Mshauri wa upanuzi wa barabara ya Mwenge hadi Tegeta kutoka kampuni ya Konoike  ya  Japan   kuhakikisha wanamaliza ujenzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 12 inayogharimu sh. bilioni 88 kwa muda unaotakiwa na kuacha kusingizio cha mvua kama wanavyodai kuwa umechelewa kwa asilimia saba.
“Mvua zilinyesha siku tatu haiwezi kuwa sababu kuna  nchi mvua inayesha muda mrefu kuliko Tanzania na ujenzi wa barabara unaendelea. Sijaridhika na hiyo sababu ninyi nchi za nje  mnaweza kujenga hata mvua ikiwa inayesha. Ni lazima wafidie muda … kuongeza kazi ya ujenzi hakutakuwa na ongezeko la muda wala mtaji,” alisisitiza.
Wakati huohuo  Waziri Magufuli alitumia nafasi kuwataka wakazi wa Jiji hilo waliojenga katika maeneo ya hifadhi za barabara hizo kuondoka wenyewe kwa kuwa sharia ni msumeno.
“ Tukikuta mradi unakwamishwa sisi tutabomoa.
Akizungumzia kuhusu mradi DART , Afisa Mtendaji wa  DART Cosmas Takule alisema utatengeneza ajira 80,000 na kusaidia abiria 406,000. Mradi huo utakamilika katika kipindi cha miezi 36.
Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dares Salaam , Mwamtumu Mahiza alitka ajira hizo ziwe kwa vijana wa jiji hilo.

No comments: