Thursday, June 28, 2012

FIESTA 2012 ITAKAYOFANYIKA MBEYA YAZINDULIWA LEADERS CLUB

Meneja wa Vipindi wa Clouds FM, Sebastian Maganga (wa pili kulia) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani). Kutoka kushoto ni Meneja wa Kampeni wa Kampuni ya Push Mobile, Rugambo Rodney, Meneja wa Kampuni ya Serengeti Premium Lager, Allan Chonjo na wa mwisho kulia ni Meneja wa Masoko wa Kampuni ya Gapco Tanzania, Ben Tema.
Mtangazaji wa Redio Clouds FM, Millard Ayo (aliyesimama) akiwa na mtangazaji mwenzake, Babra Hassan, wakiongoza sherehe hizo za uzinduzi.…
Meneja wa Vipindi wa Clouds FM, Sebastian Maganga (wa pili kulia) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani). Kutoka kushoto ni Meneja wa Kampeni wa Kampuni ya Push Mobile, Rugambo Rodney, Meneja wa Kampuni ya Serengeti Premium Lager, Allan Chonjo na wa mwisho kulia ni Meneja wa Masoko wa Kampuni ya Gapco Tanzania, Ben Tema.
Mtangazaji wa Redio Clouds FM, Millard Ayo (aliyesimama) akiwa na mtangazaji mwenzake, Babra Hassan, wakiongoza sherehe hizo za uzinduzi.
Baadhi ya zawadi ambazo zitatolewa kwa mashabiki wa burudani katika msimu huu wa Fiesta 2012.
Wasanii na wadau waliohudhuria uzinduzi huo wakiwa katika picha ya pamoja.
Magari  yatakayotolewa kama zawadi yakionyeshwa katika viwanja hivyo.
UZINDUZI wa tamasha kubwa la kila mwaka linalofamamika kama ‘Fiesta 2012’, umefanyika leo kwenye Viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam ambapo uongozi wa Clouds Media Group ulitangaza kuanza kwa shamrashamra za awali mwishoni mwa wiki hii  jijini Mbeya.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye uzinduzi huo, Meneja wa Vipindi wa Clouds FM, Sebastian Maganga, alisema tamasha hilo lenye kauli mbiu ya “Bhaaas”,  mwaka huu linatarajiwa kuibua vipaji vipya kama ilivyokuwa kwa msanii ‘anayehit’ kwa sasa, Nasibu Abdul ‘Diamond’, ambaye kwa sasa ni bonge la staa ndani ya ulingo wa Bongo Fleva.

Aidha, Maganga aliongeza kwa kusema kwamba mbali za kuibua vipaji vipya, mwaka huu zawadi zenye thamani ya shilingi milioni 150 zitatolewa kwa mashabiki ikiwa ni sehemu ya kurudisha fadhila kwa jamii.

“Tuna magari aina ya Vitz na pikipiki zipatazo 14 ambavyo vyote kwa pamoja vitarudi kwa wanajamii kama zawadi kwao,” alisema Maganga.

Uzinduzi huo wa tamasha hilo ambao unatimiza miaka 11 tangu kuanzishwa, ulihudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo wasanii  na waandashi wa habari.

                      PICHA/HABARI: ERICK EVARIST NA MUSA MATEJA /GPL

No comments: