Friday, July 20, 2012

FOUR WAYS BUKOBA BLOGS INATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO

KWA mara nyingine, Watanzania  tumepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa za kuzama kwa meli ya MV. Skagit iliyotokea jirani na kisiwa cha Chumbe, Unguja. Ndugu zetu wapatao 60 tayari wameripotiwa kupoteza uhai. Huu ni msiba mkubwa kwa taifa letu.


FOUR WAYS BUKOBA BLOGS, kama chombo cha jamii cha habari na mawasiliano kinatoa salamu za rambirambi kwa  wahanga wote wa msiba huu mkubwa. Na  tunachukua fursa hii kumpa mkono wa pole  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa  Dr.  Jakaya Mrisho Kikwete, vivyo hivyo, mkono wetu wa pole umfikie Mheshimiwa Dr. Ali Mohammed Shein, Rais wa Serikali ya Mapinduzi Ya Zanzibar.
FOUR WAYS BUKOBA BLOGS tunaungana na watu wote duniani kuwaombe ndugu zetu walipoteza maisha katiuka ajari ya kuzama kwa meli.
Imetolewa na
Mkurugenzi Mtendaji wa www.fourwaysbukoba.blogspot.com
Bw.Eliud Theobard Russeta

No comments: