Monday, July 2, 2012

MAONESHO YA KILIMO NA BIASHARA SABASABA MWAKA HUU YAZINDULIWA RASMI NA MKUU WA WILAYA YA BUKOBA.

Yanafanyika katika viwanja vya CCM ambapo washiriki mbalimbali zikiwemo Redio za mjini hapa zimeshiriki kurusha matangazo Live (KASIBANTE REDIO na VISION FM)

\
Banda la Kasibante


 
 KIKUNDI cha walemavu wa viongozi wanaojishughulisha stadi za kazi katika Manispaa ya Bukoba wameiomba serikali kuwaongezea mitaji ili kuweza kununulia malighafi.
Ombi hilo limetolewa leo na baadhi ya wanakikundi cha walemavu wa viungo wajulikanao kama East African drums Bukoba  disabled Assistance Project (BUDAP) wakati wakizungumza na blog hii katika banda lao la maonesho ya saba saba yanayofanyika mjini hapa.


Mwenyekiti wa BUDAP Bw. Issa Zacharia alisema hawapati wateja wa kununua bidhaa zao kutokana na kukaa nje ya mji na kutokuwa na uwezo wa kupanga chumba kati kati ya mji jambo ambalo linawaathiri katika biashara zao.

Alisema kikundi hicho ambacho kinajumla ya wanachama saba wote wakiwa ni walemavu wa viungo, wanakabiliwa na  ukosefu wa kupata fedha

kwa jili ya kununulia mali ghafi.

Halikadhalika mwanakikundi mwenzake ambaye pia ni mlemavu, Bw. Ashlafu Ramadhani alisema kutokana na ukosefu wa malighali inawafanya kutengeneza ngoma ndogo ambapo wakatiwa na malighafi hutengeneza ngoma kubwa ambazo hulazimika kuuza kwa sh.30,000.

No comments: