Sunday, July 22, 2012

RAIS DK SHEIN AWAONGOZA AWAONGOZI VIONGOZI NA WANANCHI KATIKA DUA YA HITMA KUWAOMBEA WALIOKUFA KWA AJALI YA MELI


 Na Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed
Shein,  leo ameungana na viongozi mbali mbali wa Kitaifa katika dua
maalum ya hitma pamoja na Sala maalum ya Maiti (Salatul Mayyit
al-ghaib), iliyosomwa huko katika msikiti Mushawar, Mwembeshauri mjini
Zanzibar.

Sala na dua hiyo ni maalum kwa ajili ya kuwaombea watu waliokufa
kutokana na ajali ya kuzama kwa meli ya MV SKAGIT,  iliyotokea hivi
karibuni wakati meli hiyo ilipokuwa inasafiri kutoka Dar-es-Salaam
kuja Zanzibar na kusababisha vifo na majeruhi kadhaa

Katika sala na dua hiyo viongozi mbali mbali wa dini, vyama na
Serikali walihudhuria akiwemo Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muunganao
wa Tanzania Mhe. Dk. Mohammed Kharib Bilal, Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Idd, Rais mstaafu wa Zanzibar Mhe. Dk.
Amani Abeid Karume.

Viongozi wengine waliohudhuria ni Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Omar
Khabh, Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji, Spika wa Baraza la
Wawakishi Mhe. Pandu Ameir Kificho, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib
Mhe. Abdalla Mwinyi Khamis, Mawaziri, Manaibu Waziri, Wabunge,
Wawakilishi, Mashekhe mbali mbali wa Zanzibar na Tanzania Bara pamoja
na wananchi na viongozi wengine.

No comments: