Thursday, August 23, 2012

AJIRA KWA WATOTO WADOGO NI ADHABU





Wakati selikari ya Tanzania na kwa ushurikiano na umoja wa mataifa wakianagaika kupunguza ongezeko la ajira kwa watoto wadogo na kuwatengenezea mazingira ya ajira bora katika ukubwa wao leo katika hekaheka zangu kamera ya www.fourwaysbukoba.blogspot.com imekutana na watoto waliokisiwa kuwa na miaka kumi na 12 wakiwa wawili wanafanya biashara ya kuuza vitumbua mitaa.
Wakati nikifanya maojiano nao walidai  kuwa bila kufanya hivyo hawataweza kupata riziki yao kwani wameagizwa kufanya kazi hilo.
Ni jambo ya kusikitisha kwani  usiku kama huu ni mda wa mtoto kupumuzika mara baada ya kusoma kutwa nzima ukiunganisha na haki yake ya kucheza.
Ni wajibu wa kila mmoja wetu kukemea jambo hili la kusikitisha kwani watoto wetu wanahitaji elimu ya kutosha ili waweze kumudu maisha yao ya baadae
Eliud
0768078360

No comments: