Wednesday, September 19, 2012

DUDE: MTITU AMENIPIGA BAO



 
Na Erick Evarist
BAADA ya Kulwa Kikumba ‘Dude’ kujinadi kwa muda mrefu kutaka kufunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu anayeishi naye Eva bila mafanikio, ameibuka na kusema: “Mtitu amenipiga bao.”
Katika mazungumzo na kona hii juzi jijini Dar es Salaam, Dude alisema: “Lazima nikiri hilo, nilitamani sana kufunga ndoa na Eva mapema zaidi, nilitaka msanii yeyote asifunge ndoa kabla yangu, lakini Mtitu amenipiku, hilo lazima nilikubali na ninajisikia aibu sana,” alisema Dude na kuongeza:
“Hata hivyo,   sijakata tamaa na haijatokea kwa makusudi....unajua kulikuwa na vipingamizi vingi upande wa mke wangu ndiyo maana nimeshindwa kufanya hivyo kwa wakati lakini tumeshaweka mambo sawa, mwakani tutaoana.”
William Mtitu aliye prodyuza na msanii wa filamu Bongo, alifunga ndoa mwishoni mwa wiki iliyopita na mkewe Yovina Swai na kufanya hafla kubwa iliyohudhuriwa na mastaa kibao

No comments: