Wednesday, September 19, 2012

MKUU WA MKOA KAGERA AKABIDHI ARUDISHA SHULE MIKONONI MWA WANCHI MLEBA

Mhe. Massawe Akiwahutubia Wananchi wa Kata ya Katoke Kabla ya Kuwakabidhi Shule yao waliokuwa wamenyanganywa na mbunge wa zamani wa jimbo la Muleba Kaskazini Ruth Msafiri iliyoko eneo la Kimbugu.
Majengo ya Shule ya Sekondari ya Wasichana ambayo Ruth Blasio Msafiri alikuwa anadai kuwa ni Mali yake, shule hiyo imekabidhiwa kwa wananchi wa kijiji cha Kimbugu kilichoko katika kata ya katoke wilayani Muleba

Mkuu wa mkoa wa Kagera Kanali mstaafu Fabian Massawe, akiwa ameongozana na wananchi wa kata ya Katoke kwenda kuwakabidhi majengo ya shule ya sekondari inayojulikana kwa jina la Ruth Msafiri, jina la aliyekuwa mbunge wa jimbo la Muleba Kaskazini, pamoja na shule hiyo kujengwa kwa nguvu ya wananchi mbunge huyo alikuwa nadai ni mali yake hadi Massawe alipoirudisha mikononi mwa wananchi. 

Aliyeruka juu akicheza ngoma sio msanii ni Mkuu wa mkoa wa kagera Kanali mstaafu Fabian Massawe, alikuwa akifurahi na wananchi wa kata ya Katoke baada ya kutatua mgogoro wa kugombania shule inayojulikana kwa jina la Ruth Msafiri. Picha na ofisi ya mkuu wa mkoa Kagera
 

No comments: