■AKATAA KUKUMBATIANA NA WAGENI WAKE UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA HOSEA KUTAKO, WINDHOEK, NAMIBIA
Mtanzania
Rajabu Maoja amelitingisha jiji la Windhoek, nchini Namibia alipoingia
katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Hosea Kutako. Maoja aliingia kwa
mbemwe za aina yake baada ya kukataa kukumbatiana na wenyeji wake ambao
walikuwa na shauku ya kumkumbatia.
Akiwa
na sura ya kujiamini huku akitembea kibabe Mtanzania Maoja alionyesha
nia ya kuuchukua mkanda wa ubingwa wa IBF katika bara la Afrika wakati
atakapoumana na bingwa wa Namibia Gottlieb Ndokosho siku ya Jumamosi
tarehe 29, Septemba.
Mpambano
huo ulipewa jina la Vita Vya Jangwa wa Kalahari (The Battle for the
Kalahari Desert) na waandaaji wake ambao ni kampuni ya Kinda Boxing
Promotions inayoongozwa na Simon Nangolo limeleta shamrashamra za aina
ya pekee katika ukanda huu wa Kusini mwa jangwa la Sahara.
Mpambano
huo ni moja ya mapambano ambayo yapo kwenye programu ya Utalii wa
Michezo ya IBF (IBF Sports Tourism) ambayo inasimamiwa na Shirikisho la
Ngumi la Kimataifa (IBF) na kuratibiwa na Rais wa IBF katika bara la
Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi, Mtanzania Onesmo Alfred
McBride Ngowi.
Nao
mabondia kutoka Zimbabwe na Afrika ya Kusini ambao watacheza mapambano
ya awali wameshafika na tayari shamrashamra za mpambano huo zimeshika
kasi kwa wadau na wapenzi wa ngumi wa nchi ya Namibia na nchi jirani
kama Botswana, Afrika ya Kusini, Lesotho na Swaziland.
Hii ni mara ya kwanza kwa ushandani mkubwa namna hiyo kuwahi kutokea katika jiji la Windhoek hapa Namibia.
Mpizania wa Maoja Gottlieb Ndokosho ameingai mitini na hajaonekana tangu tuingie katika jiji hili la maraha!
Kesho ni kesho na Watanzania wamuombee mwakilishi wao ili aweze kuipeperusha vizuri bendera ya Tanzania!
Mungu mbariki Rajabu Jumanne Maoja, Mungu ibariki nchi nzuri ya Tanzania.
Imetolewa na:
Uongozi
Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC)
No comments:
Post a Comment