Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,
Dk. Shukuru Kawambwa akimlaki Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Bi. Irina
Bokova's aliyewasili nchini usiku wa kuamkia leo kwa ziara ya kikazi ya
siku mbili nchini. Waliobaki nyuma ni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa
nchini Tanzania Dkt. Alberic Kacou, Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa
Mh. Begum Taj na Msaidizi wa Mkurugenzi wa UNESCO.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,
Dk. Shukuru Kawambwa (kulia) akimwongoza Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Bi.
Irina Bokova's sehemu ya mapumziko kwa viongozi mara baada ya kuwasili
katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere (VIP Terminal) usiku wa kuamkia leo . Bi. Irina Bokova's atakuwa nchini kwa ziara ya Kikazi ya siku mbili itakayoanza leo.
Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Bi. Irina
Bokova's akisalimiana na Katibu Mkuu wa Natcom Prof. Elizabeth Kiondo.
Wanaoshuhudia tukio hilo Mkurugenzi Msaidizi wa UNESCO Africa Bi. Lalla
Aicha Ben Barka (wa pili kushoto) na Mwakilishi wa Shirika la UNESCO
nchini Tanzania Vibeke Jensen (kulia).
Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Bi. Irina
Bokova's ( wa pili kulia) akizungumza jambo na mwenyeji wake Waziri wa
Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk. Shukuru Kawambwa. Kushoto ni Balozi wa
Tanzania nchini Ufaransa Mhe. Begum Taj na kulia ni Mwakilishi wa
Shirika la UNESCO nchini Tanzania Vibeke Jensen.
Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Bi. Irina Bokova's (katikati) akiwa
kwenye picha ya pamoja na wenyeji wake Waziri wa Elimu na Maufnzo ya
Ufundi Dk. Shukuru Kawambwa (kushoto) na Balozi wa Tanzania nchini
Ufaransa Mhe. Begum Taj.
Dk. Shukuru Kawambwa akimsindikiza mgeni wake Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Bi. Irina Bokova's.
Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Bi. Irina
Bokova's akiondoka katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl. Julius
Nyerere (VIP Terminal) mara baada ya kuwasili nchini Tanzania usiku wa
kuamkia leo kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.
No comments:
Post a Comment