WATANO WAFARIKI NA 130 WAJERUHIWA VIBAYA KATIKA AJALI YA ROLI WALILOKUWA WAKISAFIRIA KWENDA SHAMBA KAPUNGA MBARALI MBEYA
MOJA YA MTOTO MAJERUHI AKIHAMISHWA KUTOKA KATIKA HOSPITALI YA MISION CHIMARA NA KUPELEKWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA
MOJA YA MAJERUHI AKISUBIRI KUPATA MATIBABU
HILI NDILO ROLI WALIMOPANDA VIBARUA HAO WA SHAMBA LA KAPUNGA
KWELI MUNGU NI MKUU HUWALINDA WATOTO WADOGO HAPA MKUU WA MKOA AKIMPA MOJA YA WATOTO WALIOPATA AJALI
HUYU BINTI NI MWANAFUNZI NAE ALIKUWEPO KWENYE AJALI HIYO
MKUU WA MKOA MBEYA ABAS KANDORO AKIONGEA NA WAANDISHI WA HABARI
MAJERUHI 22 WAKIPAKIZWA KATIKA ROLI AINA YA FUSO TAYARI KUPELEKWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA
MAJERUHI WAKISAFIRISHWA KWENDA MBEYA
MWANDISHI WETU JOSEPH MWAISANGO AKITOKA KATIKA HOSPITALI YA CHIMALA BAADA YA KUSHUHUDIA NA KUPATA HABARI ZA UHAKIKA MAANA TAARIFA YA AWALI ILITOLEWA KUWA WATU WASIOZIDI 30 WAHOFIWA KUFA KATIKA AJALI SASA TUNAHABARI KAMILI BAADA YA MBEYA YETU KUFIKA KATIKA TUKIO
WATU watano wamepoteza maisha na wengine 130 wamejuruhiwa vibaya huku hali zao zikiwa mbaya baada ya Lori walilokuwa wakisafiria shambani kuacha njia na kupinduka katika kijiji cha Mapogolo kata ya Itamboleo Wilayani Mbarali Mkoani hapa.
Ajali hiyo imetokea leo saa 1:30 asubuhi ambapo lori hilo ambalo ni mali ya Mwekezaji wa shamba la Kapunga Rice Project, na kwamba watu hao walikuwa wakielekea kwenye shamba la mwekezaji huyo lililkuwa limebeba vibarua hao zaidi ya 200 ambao ni wakazi kitongoji cha Kapunga.
Lori hilo lenye namba za uasjili T398 BSE Scania Tipa, ambalo lilikuwa likiendeshwa na dereva aliyejulikana kwa jina Baraka Moreli, lilionekana likiwa katika mwendo kasi na dereva huyo akiwa na lengo la kutaka kuipita pikipiki iliyokuwa mbele yake. huku akishangiliwa na vibarua hao ipite ipite hiyo pikipiki haiwezi kutushinda sisi gari kubwa moja ya majeruhi alisema. ndipo walipofika kwenye kona dereva lilimshinda gari hilo na kupinduka
Akiwa Hospitalini hapo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro ambaye aliweza kufika hospitalini hapo alisema kuwa mara baada ya kupata taarifa ya ajali hiyo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya ,Mbarali Gullam Hussein Kiffuu, huku akiombwa kupatiwa msaada wa kuongezewa madaktari, kuongezewa vifaa vya mataibu sambamba na uwezekano wa kupata damu kwa ajili ya kuwaongezea majeruhi hao alifanikiwa kuwasiliana na uongozi wa hospitali ya Rufaa ya Mbeya, hospitali ya Mkoa ili kuweza kuona namna ya kwenda kuokoa maisha watanzania hao.
Kandoro, alisema kuwa katika ajali hiyo wanaume wanne wamefariki na mwanamke mmoja. watatu wametambuliwa
Samweli Mapugilo mbena 30 mkazi wa Ilembula
Bon Mfupa 27 mkazi wa mapogolo na Edgar Mwakipesile 35 mkazi wa Nonde Mbeya Aidha, Kandoro alisema kuwa idadi ya majeruhi katika ajali hiyo kuwa ni 130 ambapo wanawake ni 40 na wanaume 89 huku idadi ya watoto waliokuwa wameongozana na wazazi wao haikuweza kufahamika kwa haraka.
Pcha Mbeya yetu na Kamanga
No comments:
Post a Comment