Na: Albert Sanga, Iringa.
Leo
nina neno na wafanyakazi waliopo katika sekta mbalimbali; za umma na za
binafsi. Nimeamua kuandika waraka huu wa uchumi leo kwenda kwa
wafanyakazi kutokana na sababu kuu tatu. Mosi, uwepo wa mbinyo wa
kuongezeka kwa gharama za maisha ikilinganisha na vipato halisi vya
wafanyakazi. Pili, kuwepo kwa uwezekano wa wafanyakazi kujikwamua
kiuchumi kupitia ujasiriamali. Tatu, hata kama wafanyakazi wasipoona
umuhimu wala ulazima wa kuongeza vipato vyao; bado wafanyakazi ni moja
ya
kundi linaloweza kuliokoa taifa hili kwa kutengeneza maelfu ya ajira ikiwa wataamua kufanya hivyo.
Wafanyakazi
wengi (japo yaweza kuwa sio wote) watakubaliana na mimi ya kwamba
mishahara na marupurupu yanayotolewa ajirani hayatoshelezi mahitaji ya
kimaisha. Gharama za maisha zimekua juu, mfumuko wa bei unazidi kutikisa
nchi na imefika mahali watu hawaelewi waishi vipi.
Upandaji
wa maisha hauendani na ongezeko la mshahara, malengo ya kimaisha sio tu
kwamba hayatimii; lakini hayawezi kutimia kama mtu utaendelea kutegemea
namna ile ile ya kipato-mshahara na marupurupu.
Yapo
mambo mawili ningependa kila mfanyakazi afahamu. Cha kwanza ni kuwa;
mabadiliko tunayoshuhudia nchini, ikiwemo kupanda kwa gharama za maisha
na mfumuko wa bei ni mabadiliko ambayo yanaukumba ulimwengu mzima na sio
Tanzania pekee.
Kwa
maana hiyo, utatuzi wa suala hili ni kuachana na kufikiria kienyeji
(local thinking) badala yake watu tufikirie kiupana (global thinking).
Sambamba na hilo ni vema mtu mmoja mmoja kuwa na mtazamo chanya kuhusu
ramani ya maisha kwa ujumla.
Cha
pili ni kuwa; siasa haziwezi kuamua hatma yako isipokua umeziruhusu
kufanya hivyo. Labda niiseme falsafa yangu kuhusu siasa ndipo naweza
kueleweka zaidi; "Politics has nothing to do with my destiny". Maana ya
falsafa yangu hii ni kwamba siasa zinaweza kunizuia kwa muda kufika
ninakotaka, lakini haziwezi kunizuia milele.
Nikisema
hivi simaanishi ninaukana umuhimu wa siasa katika ustawi wa kiuchumi
kwa wafanyakazi na mtu mmoja mmoja. Isipokuwa ninachotaka turekebishe ni
ile hali ya kudhani siasa zitafanya kila kitu maishani mwetu.
Nimeyataja
mambo hayo mawili ili kusafisha njia ya kuelekea kwenye fikra pevu
kuhusu uhuru wa kiuchumi kwa wafanyakazi. Kila mfanyakazi ni vema
akafahamu kuwa usalama wa maisha yake hauwezi kuletwa na ongezeko la
mshahara. Bila kulitambua na kulikubali hili tunaweza kuwa shidani; kwa
sababu mara nyingi mtaji wa wanasiasa kupatia kura huwa ni ongezeko la
mishahara!
Wanauchumi
tunafahamu vizuri mchezo unaotokea pindi serikali inapoongeza
mishahara, pasipo kuongeza tija ya uzalishaji. Iko hivi, unapoongeza
mzunguko wa fedha, (unbalanced injection of money into circulation)
mfano kwa kuongeza mishahara kinyume na mizania ya kiuchumi; ikiwa
hakuna tija katika uzalishaji basi unakuwa ukiibua mfumuko wa bei
(inflation).
Kuanzia
mataifa madogo mpaka makubwa hadi nikiandika makala hii yanasumbuliwa
na kusuasua kwa uchumi. Wanapojaribu kushusha 'inflation' wanajikuta
wametengeneza uhaba mkubwa wa ajira, wanapojaribu kumimina ajira mitaani
wanajikuta mfumuko wa bei unainua pembe zake.
Hata
hivyo nikiri kuwa inawezekana kuleta msawazo wa ujazo wa fedha na
mfumuko wa bei; lakini kufanikiwa kwake kunategemea visababishi vingi
mno (simulation factors) ambavyo kutokana na utamaduni wa nchi yetu
kiuchumi; sio rahisi kuvifanikisha vyote. Yote katika yote; hizo ni
lugha na misamiati ya wachumi; lakini ni nini maana yake kwa mfanyakazi?
Hayo
juu yanatupa kutambua kwamba kumbe usalama wa maisha ya mfanyakazi
utapatikana kwa kujifunza mbinu za kuutumia mshahara kidogo anaoupata
kuzalisha mifumo, bidhaa na huduma zitakazomwongezea tija. Hili linaweza
kufanikishwa kwa mfanyakazi kuanzisha miradi midogo midogo nyumbani au
mikubwa mahali pengine, kufungua biashara na hata kutumia vipawa
alivyonavyo nje ya ajira yake kuzalisha fedha.
Nianze
sasa na yale mambo matatu yaliyonisukuma kuwaandikia waraka huu,
nikianza na lile la kwanza. Udogo wa mishahara isiyoendana na gharama za
maisha unazidi kuleta msiba katika nchi yetu.
Hebu
fikiria, mfanyakazi analipwa mshahara mdogo ambao akishalipa kodi ya
nyumba, akanunua chakula, akafanya matumizi mengine ya msingi; kila
mwisho wa mwezi anajikuta ana madeni. Tangu Januari hadi Desemba
mfanyakazi huyu anakua ni mtu sio tu wa madeni ila ni madeni
yanayoongezeka. Hana tumaini la kujikwamua kesho wala keshokutwa.
Kutokana
na hali hii tumezalisha wafanyakazi wengi ambao wajibu wao wameugeuza
kama hisani makazini, ndio hawa ambao hawawezi kukuhudumia mpaka umewapa
chochote. Wengine wameendelea 'ku-survive' kwa kuunga unga, wanaishi
kwa mizinga kila wakati na kila sehemu. Huwezi kuwalaumu; wanalazimishwa
na mazingira yanayowakabili.
Nchi
sasa hivi imejipatia 'mamilionea' bandia ambao wamepata fedha zao kwa
njia ya kughushi mikataba, kupewa hongo, kupokea rushwa kubwa na ndogo
pamoja na wizi wanaoufanya makazini. Wakishapata fedha hizo ndipo
wanajenga majengo makubwa makubwa, wananunua magari ya kifahari na
kuishi maisha ya kifalme. Wengi wetu tumeingia katika mtego wa kuwasifu
watu wa namna hii ya kwamba ni 'wajanja', 'watafutaji', 'wenye akili',
'matajiri' na majina mengine yenye sifa.
Kuna
atahri mbili kubwa mfanyakazi unaposhawishika kupata mafanikio kwa njia
zisizo halali. Mosi ni kwamba unaliangamiza taifa na kuwadhulumu
wengine. Pili, unaharibu utu wako wa ndani na kupoteza amani ya rohoni.
Iko hivi; kikawaida uovu humrudia muovu, wema humrudia mwema.
Ukijikusanyia
mali ama fedha kwa njia ya wizi, rushwa, hongo ama ujanja-ujanja;
utajikuta unaishi maisha yasiyokua na amani kunakopelekea kukosekana kwa
furaha maishani mwako. Kikawaida mtu unapaswa uwe na mafanikio
yanayoleta utulivu katika roho na nafsi yako; kinyume na hapo haina
maana ya kuwa na mafanikio.
Najua
wapo watu mnaowafahamu ambao wametajirika kwa njia za mikato; nanyi
mnaona kama wanaishi maisha mazuri yenye furaha; ukweli wanaujua wenyewe
kama ambavyo tunathibitishiwa na wataalamu wa ukuaji wa kiroho,
saikolojia na maumbile; ya kwamba uovu humrudia mwovu.
Unaweza
kutumia rushwa kutajirika lakini malipo ukayapata kupitia mgogoro wa
ndoa na kudharaulika; ndio maana huwa sishangai ninapoona watu wengi
wakitafuta furaha kupitia ngono na ulevi; wengi wao njia walizotumia
kupata mafanikio waliyonayo zimewapa 'garantii' ya kutokua na furaha
maisha yao yote!
Kwa
nini ninasema haya yote? Ni kwa sababu ninataka tuangalie upande wa
pili ya kwamba tupende ama tusipende ni lazima wafanyakazi wote
wafanikiwe ili kukabiliana na yanayowakabili maishani; lakini
mnafanikiwaje? Ndipo hapo ambapo ninataka tuyaone maisha katika mwanga
wa ujasiriamali. Tuonane kwenye sehemu ya pili ya waraka huu.
Kila mfanyakazi anastahili kuishi maisha ya ushindi wa kiuchumi!
stepwiseexpert@gmail.com; 0719 127 901
stepwiseexpert@gmail.com; 0719 127 901
No comments:
Post a Comment