Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (wapili kushkto)
akizungumza na Wabunge kutoka kulia, John Cheyo Bariadi Mashariki (UDP), James
Mbatia wa kuteuliwa (NCCR Mageuzi) na
Mansoor Shanif Hiran mbunge wa Kwimba
(CCM) nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma jana.Kushoto ni Mkurugenzi wa Msama
Promotion, Alex Msama.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda, (kulia) akizungumza na Mkurugenzi wa Msama
Promotion, Alex Msama nje ya Ukumbi wa Bunge mjini DodomaJuni 27,2013.
Naibu
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makalla (kulia)
akifurahia jambo na Mbunge wa Mbeya Mjini na Waziri Kivuli wa Wizara hiyo
kutoka Kambi ya Upinzani Bungeni, Joseph Mbilinyi nje ya Ukumbi wa Bunge mjini
Dodoma jana.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Dk.Terezya Huvisa
akisisitiza jambo wakati akiongea na wapigapicha za Habari nje ya Ukumbi
wa Bunge mjini Dodoma leo. Mazungumzo makubwa yalikuwa juu ya Usafi
hasa jiji la Dar es Salaam. Dk. Huvisa alisema jiji sasa litakuwa safi
na tayari mkakati wao umekutana na ziara ya Rais Obama wa Marekani hivyo
utakuwa endelevu
Waziri
Kivuli wa Maji na Umwagiliaji, Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Sabreena
Hamza Sungura akizungumza na Mbunge Mwenzake nje ya ukumbi wa Bunge.
Mbunge wa Mafia ambaye
pia ni Kamishna wa Skauti Tanzania, Abdulkarim Shah, akizungumza na vijana wa
Skauti Mkoa wa Dodoma waliotembelea Bungeni jana kujifunza shughuli mbalimbali.
Wabunge ni wachache bungeni maana imesalia siku moja kwa Bunge kuahirishwa...
Mbunge wa Viti Maalum, Paulin Gekul akisoma ratiba ya Shughuli za Bunge Juni 27,2013.
Mbunge
wa Jimbo la Ilala, Mussa Zungu Azzan (kushoto) na Mbunge wa Jimbo la
Kinondoni, Iddi Mohamed Azzan wakiwa Bungeni Dodoma.
Halima Mdee Mbunge wa Jimbo la Kawe akigeuka kuzungumza na Wabunge wenzake wa CHADEMA Bungeni.
Mbunge wa jimbo la Kawe,
Halima Mdee (kushoto) na Mbunge wa viti
Maluum, Paulin Gekul wakiwa Bungeni. Nyuma ni Mbunge wa Viti Maalu, Chiku Abwao.
Wabunge mbalimbali wa CHADEMA wakiwa Bungeni
Mbunge
wa Viti Maalum, Dk. Mary Mwanjelwa (kushoto) Mbunge wa Viti Maalum,
Lediana Chilolo (katikati) na Mbunge wa Uzini Mohamed Seif Khatib wakiwa
nje ya Ukumbi wa Bunge.
No comments:
Post a Comment