Mlinda Mlango Deogratius Mushi 'Dida' akifanya mazoezi na wachezaji wenzake wa Yanga, Loyola Sekondari hii leo.
KIPA mpya aliyesajiliwa na
mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga SC, Deogratius Munishi
'Dida' pamoja beki wa kati aliyesajiliwa kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro, Rajab
Zahir leo wameanza rasmi mazoezi na timu yao Uwanja wa sekondari ya Loyola,
Mabibo, Dar es Salaam.
Deogratius Munishi 'Dida' ameungana na wachezaji wengine wawili mshambuliaji Shaban Kondo aliyekua akicheza soka nchini Msumbiji pamoja na Zahir aliyerejea kutoka nchini Afrika Kusini alipokuwa akifanya majaribio katika timu mbili za Ligi Kuu nchini humo.
Mapema jana katika siku ya kwanza
ya mazoezi kiungo mshambuliiaji Mrisho Khalfan Ngassa alifanya mazoezi asubuhi
chini ya kocha mholanzi Ernest Brandts kabla ya kocha huyo kuwapa nafasi
wachezaji wote wa timu ya taifa, Taifa Stars kujiunga na timu hiyo leo kwa
ajili ya maandalizi ya mchezo dhidi ya Uganda julai 13 Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Hadi sasa klabu ya Yanga
imefanikiwa kusajili wachezaji watano wapya ambao ni Dida kutoka Azam, Zahir wa
Mtibwa, Ngassa wa Simba, Shaban Kondo aliyekuwa Msumbiji na Realitus Lusajo
kutoka Machava FC.
Kocha Brandts amefurahia kuongezeka kwa wachezaji
hao kwani amesema atapata fursa ya kukaa nao na kucheza michezo ya kirafiki
kanda ya ziwa hali itakayopelekea kupata nafasi ya nzuri kukiandaa kikosi na
msimu mpya wa 2013/2014.
Yanga itaendelea na mazoezi kesho asubuhi Loyola
ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya ziara yake Kanda Ziwa inayotazamiwa kuanza
mwishoni mwa wiki jijini Mwanza.
Wachezaji wote wameendelea na mazoezi leo asubuhi isipokua wachezaji waliojiunga na kambi ya timu ya Taifa kwa ajili ya mchezo dhidi ya Uganda.
No comments:
Post a Comment