Friday, August 9, 2013

yanga yawatandika 1-0 wanaigeria '3pillars'


3PILLARSNAYANGA6 30a97
Hussein Javu akiitoka ngome ya 3 pillars (HM)

3p 88e7e
Kikosi cha 3 Pillars
MSHAMBULIAJI mpya wa Yanga SC, Hussein Javu leo amefunga bao lake la pili tangu ajiunge na klabu hiyo majira haya ya joto, akitokea Mtibwa Sugar ya Morogoro baada ya kuiwezesha timu yake hiyo mpya kushinda 1-0 dhidi ya 3Pillars ya Nigeria, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Hilo linakuwa bao la pili kwa Javu tangu atue Yanga akifunga katika mechi mbili mfululizo, baada ya mchezo uliopita dhidi ya Mtibwa Sugar kufunga bao moja akitokea benchi kipindi cha pili, Yanga ikishinda 3-1, mabao mengine yakifungwa na Jerry Tegete na Said Bahanuzi, wakati la timu yake ya zamani lilifungwa na Shaaban Kisiga 'Malone'.
 
Katika mchezo wa jana, mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara Young Africans waliingia uwanjani kwa lengo la kusaka ushindi na kuendeleza rekodi ya ushindi katika michezo ya kirafiki ya kujipima nguvu inayocheza kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom 2013/2014.

Ikiwa tumia washambuliaji wake wapya Hussein Javu na Mrisho Ngassa waliojiunga na kikosi msimu huu, Yanga ilikosa nafasi za wazi za kufungua kupitia kwa washambuliaji hao ambao hawakuonekana kuwa makini makini katika umaliziaji wa mipira iliyokuwa ikiwafikia.
 
David Luhende alikosa bao dakika ya 34 kufuatia mpira alioupiga kuokelewa na mlinda mlango wa 3Pillars FC na kuwa kona ambayo haikuzaa matunda, huku awali Said Bahanuzi akikosa nafasi pia kama hiyo dakika ya 17 ya mchezo.
 
Hussein Javu aliipatia Young Africans bao kwanza dakika ya 40 ya mchezo kwa ustadi akiitumia vizuri nafasi hiyo aliyopewa na kuingo Athuman Idd 'Chuji' aliyewazidi ujanja walinzi wa 3Pillars FC na kumpasia Javu aliyeukwamisha mpira wavuni na kuhesabu bao kwa watoto wa Jangwani.

Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika, Young Africans -0 3Pillars FC. Chanzo: binzubeiry

No comments: