Marekani imesema kuwa kundi
wapiganaji wanamgambo wa Islamic State( IS) ni hatari kwa usalama wa
mataifa mengi katika kanda ya Mashariki ya Kati na washirika wake katika
Mataifa ya Magharibi.
Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Chuck Hagel,
amewataja wapiganaji hao wa IS kuwa kundi lisiloeleweka na linazidi
kundi lingine lolote lile la kigaidi.
Hata
hivyo hakuna kilichosemwa kuhusu hatua ilizochukuliwa na jeshi la
Marekani zaidi ya mashambulizi ya angani yaliyoagizwa na Rais Obama.
Marekani imeanza uchunguzi wa mauaji ya kikatili ya mwanahabari wa nchi hiyo , James Foley, na wapiganaji wa Kiislamu.
Kundi hilo limechukua sehemu kubwa ya Iraq
Bwana Hagel ameonya kuwa kundi hilo lililoteka
sehemu kubwa ya kaskazini mwa Iraq na sehemu ya Syria lazima likabiliwe
vilivyo ilikuepusha Marekani na uharibifu.
Amiri jeshi wa Marekani Martin Dempsey naye ameonya kuwa lazima kikundi hicho kikavamie katika makao yake makuu huko Syria.
Bwana Hagel amedhibitisha kuwa makomando wa jeshi la Marekani walijaribi kumuokoa mwandishi wa kimarekani lakini wakashindwa.
Wapiganaji hao wa IS walikuwa wameitisha dau la dola milioni 132 ilikumuachilia huru mwandishi huyo wa habari.
Generali Dempsey alisema kuwa kundi hilo
linaufadhili unaozidi matarajio ya Wamarekani na kuwa linauwezo mkubwa
wa kijeshi baada ya kuteka silaha walizowapokonya majeshi ya wamarekani
mbali na silaha walizotwaa walipoteka kambi mbili za majeshi ya Iraq
kaskazini mwa taifa hilo majuzi.
Aidha Jeshi hilo liliteka kambi ya jeshi la Syria vilevile na kujizolea silaha za kisasa.
''hilo ndilo tatizo letu wanapesa kutokana na
uporaji wa mabenki uuzaji wa mafuta kaskazini mwa Iraq mbali na
wafadhili katika mataifa ya Ghuba.
Ni lazima tutakabiliana nao ikiwa si sasa muda utawadia tu.''
hata hivyo wadadisi wa maswala ya Iraq walisema kuwa wote wawili hawakutangaza badiliko la kampeini yao huko Iraq.
Mapema wiki hii rais Obama alikuwa amesema kuwa
wataishambulia IS bila ya kutuma wanajeshi wa nchi kavu Iraq lakini
inavyoelekea sasa huenda Marekani ikaanza kupanga mikakati ya
kuinyamazisha IS nchini Iraq na pia Syria
No comments:
Post a Comment