…
Shakoor Jongo na Erick Evarist
MAMA wa marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa (pichani) juzikati alijikuta akiangua kilio upya wakati alipokuwa akipokea shilingi milioni 10 kutoka kwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Mhe. Amos Makalla kama rambirambi kutoka serikalini.
Akikabidhi fedha hizo, Mhe. Makalla alisema serikali imefikia hatua hiyo kutokana na mchango mkubwa wa marehemu Kanumba kwa jamii na serikali kwa ujumla enzi za uhai wake.

“Kanumba alikuwa na mchango mkubwa kwa jamii na serikali kwa ujumla ndiyo maana tumeamua kufanya hili. Nashangaa tu kusikia baadhi ya watu wakidai marehemu alikuwa mfuasi wa chama cha upinzani.
“Mimi sikubaliani na hilo kwani katika watu waliokuwa wakihamasisha kufunguliwa kwa tawi la CCM nchini Uingereza, marehemu alikuwa miongoni mwao na ndiyo urafiki wetu ulipoanzia,” alisema Makala.

Akizungumza na Risasi Jumamosi mara baada ya kupokea fedha hizo, Mama Kanumba alisema anaishukuru serikali na kuongeza kuwa, rambirambi hiyo imemtonesha kidonda cha kuondokewa na mwanaye kipenzi.
Alisema tangu mwanaye huyo afariki dunia amekuwa ni mtu wa kulia kila siku huku akiamini kuwa, atakuwa ni mtu wa kufuta machozi kwa siku 365.

“Naishukuru sana serikali kwa rambirambi hii lakini kwa kweli kila ninapokumbuka kifo cha mwanangu, machozi hayaishi kunitoka, itanichukua muda kusahau,” alisema Mama Kanumba.
No comments:
Post a Comment