Mshambuliaji wa Ivory Coast, Salomon Kalou (kulia) akipambana na Shabani Nditi wa Taifa Stars wakati wa mechi ya kuwania nafasi ya kushiriki kombe la dunia 2014 katika uwanja wa Felix Houphouet Boigny jijini Abidjan jana. Ivory Coast walishinda 2-0.
Beki wa Ivory Coast, Kolo Toure (kulia) akimdhibiti Mbwana Samatta wa Taifa Stars wakati wa mechi ya kuwania nafasi ya kushiriki kombe la dunia 2014 katika uwanja wa Felix Houphouet Boigny jijini Abidjan jana. Ivory Coast walishinda 2-0. (PICHA ZOTE KWA HISANI YA AFP)
TIMU ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, imeanza vibaya safari yake ya makundi katika kuwania nafasi ya kucheza kombe la dunia huko Brazil 2014.
Katika mchezo wake wa kwanza dhidi ya Ivory Coast uliochezwa jijini Abijan jana, imejikuta ikifungwa bao 2-0. Magoli ya Ivory Coast yalifungwa na wachezaji Solomon Kolou 18′ na Didier Drogba 80′. Wachezaji hawa wakiwa wanachezea timu ya Chelsea iliyochukua ubingwa wa UEFA 2012.
Taifa Stars ilijikuta ikicheza pungufu baada ya Agrey Morris kutolewa kwa kadi nyekundu.
Gambia nao walitoa sare ya 1-1 dhidi ya Morocco, hivyo kugawana pointi moja moja. Kwa matokeo haya, Taifa stars inashika mkia katika kundi C ikiwa haina pointi hata moja.
Tanzania itacheza na Gambia Juni 10 jijini Dar es Salaam, wakati Ivory Coast itakuwa ugenini Juni 9 dhidi ya Morocco.
No comments:
Post a Comment