Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Rais Somalia Mheshimiwa Sheikh Shariff Sheikh Ahmed leo Mei 4, 2012 kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro, baada ya mgeni huyo kuhitimisha ziara yake ya siku mbili nchini. Rais huyo wa Somalia alikuja nchini kwa mazungumzo na Mheshimiwa Rais Kikwete ambapo alitoa shukurani zake kwa Tanzania kutokana na misaada mbalimbali ya kibinadamu iliyopata na inayoendelea kupata pamoja na kuisemea vyema Somalia katika medani za Kimataifa na za Kikanda kila alipopata nafasi hiyo. PICHA NA IKULU
No comments:
Post a Comment