Thursday, April 5, 2012

Godbless Lema aenguliwa Ubunge: Hivi sasa Arusha Mjini haina Mbunge


Godbless Lema avuliwa Ubunge Arusha Mjini

MAHAKAMA Kuu Kanda ya arusha leo imemvua Ubunge aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema kwa tiketi ya CHADEMA.

Taarifa kutoka jijini Arusha zinasema uamuzi huo umefikiwa leo asubuhi Aprili 5, 2012 mbele ya Jaji Mfawidhi wa Kanda ya Sumbawanga, Gabriel Rwakibarila katika hukumu ya kesi ya kupinga matokeo ya Ubunge Jimbo la Arusha hilo yaliyo wasilishwa na wanachama watatu wa CCM waliotaka Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kutengua ushindi wa Mbunge huyo. 


Wana CCM hao waliofungua kesi hiyo ni pamoja na Mussa Mkanga (55), Happy Kivuyo (49) na Agnes Molle (44).


Lema katika Uchaguzi huo alikuwa akichuana vikali na Mgombea wa CCM, Dk. Batilda Salha Buruiani ambaye kwa sasa ni Balozi wa Tanzania nchini Kenya.

Kuvuliwa Ubunge kwa Lema, kuna kuja siku chache wakati bado cham hicho kipo katika shamra shamra za ushindi wa Ubunge jimbo la Arumeru Mashariki mkoani humo.

Pia habari za ndani ya Chama cha Chadema zinasema kuwa tayari Chama hicho kilisha soma alama za nyakati mapema katika kesi hiyo miezi kadhaa nyuma na kujipanga endapo mbunge huyo atavuliwa wadhifa wake nani kimsimamishe kutetea kiti hicho.

Habari hizo zinadai kuwa Chadema kimepanga kumsimamisha Katibu Mkuu wa Chama hicho na Mgombea Urais wa 2010, Dk. Wilbroad Silaa kutetea kiti hicho.



Wanachama hao wanadai kuwa taratibu za maadili ya uchaguzi zilikiukwa  wa kuwa mshindi alitumia lugha za kashfa, matusi na kejeli katika mikutano ya kampeni aliyofanya jimboni Arusha.

Katika kesi hiyo wadai walileta mashahidi 14 kwenda kutoa ushahidi wao katika mahakama hiyo nawadaiwa walifanikiwa kuwaleta mashahidi 5 kujitetea.


  Taarifa ya habari ya TBC saa saba mchana.
Godbless Lema anapaswa kulipa gharama zote za kuendesha kesi hii.
Aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kupitia CHADEMA, amepoteza kiti hicho kwa kuenguliwa na Mahakama katika kesi iliyokuwa inamkabili ya kupinga ubunge wake alioupata mwaka 2010 kupitia Uchaguzi Mkuu.


Kesi hiyo iliyofunguliwa na makada watatu wa CCM, Mussa Mkanga (55), Happy Kivuyo (49) na Agnes Mollel (44)  ambao walikuwa wanamtuhumu Mbunge huyo kwa kutoa kauli za udhalilishaji, matusi na kashifa kwa aliyekuwa mgombea wa Ubunge jimbo hilo kwa tiketi ya CCM, Dkt. Batilda Buriani.

Hukumu hiyo iliyosomwa na  Jaji Mfawidhi wa Kanda ya Sumbawanga, Gabriel Rwakibarila.

Katika hukumu hiyo, Lema hakuondolewa haki ya kugombea ubunge huo kwa kuwa kosa lililomtia hatiani ni matumizi mabaya ya lugha tofauti na ilivyodhaniwa kuwa ni vitendo vya rushwa. Uamuzi wa kugombea ama kutokugombea kiti hicho tena utatokana na maamuzi yake mwenyewe na ridhaa ya chama chake ikiwa kitamteua na kumpitisha kugombea.

Taarifa za watu wa karibu zinasema kuwa Lema hatakata rufaa mahakamani juu ya hukumu ya kesi hiyo, bali atakata rufaa kupitia kura ya wananchi wa Arusha Mjini wakati wa kugombea kiti hicho.

Hivyo tutarajie uchaguzi mpya ndani ya siku 90. Tanzania, nchi ya uchaguzi kila uchao...!

Kweli tunahitaji Katiba Mpya yenye kukidhi haja na inayoendana na wakati.
Maandamano ya wafuasi na wanachama wa CHADEMA wakimsindikiza "Aliyekuwa mbunge wao" kuelekea viwanja vya Ngarenaro ambapo anahutubia wananchi sasa hivi

No comments: