Wednesday, April 11, 2012

LULU APANDISHWA KIZIMBANI LEO

 

Pichani: Elizabeth Michael ‘Lulu’ akiwa katika Mahakama ya Mwanzo Kinondoni, Dar es Salaam mwaka jana alipokuwa akituhumiwa kumshambulia kwa matusi ya nguoni, mlalamikaji Kilakhaba Aziz. Richard Bukos na Issa Mnally
Msanii maarufu wa filamu hapa nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’ leo amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu jijini Dar es Salaam na kusomewa shitaka la mauaji.  
Lulu alipandishwa kizimbani kwa usiri mkubwa akitokea Kituo cha Polisi cha Oysterbay alikokuwa akishikiliwa na kupandishwa kizimbani moja kwa moja bila kuwekwa mahabusu ya mahakama hiyo kama iwavyo kwa washitakiwa wengine wanaosubiri kusomewa kesi zao.
Baada ya kupandishwa kizambani alisomewa shitaka lake na Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama hiyo, Elizabeth Kaganda ambapo alisema Mnamo Aprili 7 mwaka huu majira ya saa saba za usiku maeneo ya Sinza Vatican jijini Dar es Salaam Elizabeth Michael (18) alimuua Steven Kanumba. Katika kesi hiyo mshitakiwa hakutakiwa kujibu lolote isipokuwa alinyoosha kidole na kupinga umri uliotajwa kuwa ana miaka 18 na kusema umri wake ni miaka 17. Baada ya kusomewa shitaka hilo, Lulu alipelekwa gerezani Segerea na kesi yake itasikilizwa tena aprili 23 mwaka huu.

ALICHOELEZA LULU POLISI HIKI HAPA


Elizabeth Michael (Lulu), ameiambia polisi
kuwa kifo cha Steven Kanumba kimetokana na ugonvi kati yao, huku taarifa nyingine zikieleza kuwa huenda Lulu akafikishwa mahakamani leo.

Habari zilizopatikana jana kutoka Kituo cha Polisi Oysterbay zilieleza kuwa, Lulu alisema kuwa kulitokea ugomvi kati yake na Kanumba baada yeye kuzungumza na simu
kutoka kwa mtu maarufu anayetajwa kuwa mpenzi wake.

“Lulu alisema kuwa ugomvi ulitokana na simu aliyopigiwa na mpenzi wake mwingine, ambaye ni mtu maarufu nchini, ndipo
Kanumba akamfokea na ndiyo ugomvi ukaanzia hapo,” chanzo hicho kimesema.

Chanzo hicho kiliongeza kuwa baada ya Kanumba kuanguka, Lulu alitoka nje na kuondoka kwa gari lake hadi maeneo ya Coco Beach, lakini baadaye daktari wa Kanumba alimpigia simu akimtaka arudi ili wampeleke hospitali.

“Alipororudi Sinza ndipo akakamatwa, lakini walikuja Kituo cha Polisi Oysterbay kuchukua PF3,” kilisema chanzo hicho.

Chanzo kiliongeza kuwa tangu Lulu alipofikishwa kituoni hapo amekuwa mtulivu asiye na wasiwasi wowote hata katika mahojiano na polisi.

Katika hatua nyingine, Polisi wa kituo hicho jana walipata wakati mgumu baada ya kuibuka kundi la vijana waliotokea makaburi ya Kinondoni kumzika Kanumba, walioandamana wakidai wanamtaka Lulu.

“Tunataka jembe letu”, waliimba vijana hao waliofikia 100 wakitokea Barabara ya Ali Hassan Mwinyi huku wakishika majani na kufanya askari waliokuwapo kituoni hapo kuwahi kuchukua silaha na mabomu ya machozi kujiandaa kutuliza ghasia kama zingezuka.

Hata hivyo vijana hao walitawanyika baada ya kuona askari wakiwa tayari kupambana nao na kukimbia maeneo mbalimbali.
Katika hatua nyingine Patricia Kimelemeta anaripoti kuwa,
Msanii Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu huenda akafikishwa mahakamani leo kujibu tuhuma za kuhusika na kifo cha Steven Kanumba.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela aliliambia gazeti hili jana kuwa Lulu atafikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni mara baada ya polisi kupata ripoti ya vipimo kutoka Mkemea mkuu wa Serikali.

“Tunasubiri ripoti ya Mkemia Mkuu kubaini chanzo cha kifo hicho kwa sababu wamechukua baadhi ya sampuli za marehemu kwenda kupima na kwamba tutakabidhiwa leo(jana). Kimsingi tukipata tu taarifa hiyo tutamfikisha mahakamani,” alisema Kenyela.

Aliongeza ripoti hiyo itaweza kuwasaidia kuandika mashtaka ili yaweze kufikishwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kwa ajili ya kumfikisha mahakamani.

Kamanda Kenyela alisema kuwa, ripoti ya madaktari imewasilishwa juzi na kwamba imeonyesha kuwa Kanumba amefariki kwa ugonjwa wa mtikisiko wa ubongo.

No comments: