Thursday, April 19, 2012

Mama Salma Kikwete alipotembelea Hospitali ya watoto ya kansa nchini Brazil

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi wa Hospitali ya watoto wanaougua ugonjwa wa kansa Marli Aparecide dos Santos mara baada ya kumaliza ziara yake ya kutembelea hospitali hiyo iliyopo mjini Brasilia nchini Brazili. Hospitali hiyo inatibu asilimia sabini ya kansa na hivyo kuwawezesha wagonjwa ambao ni watoto  kuendelea kuishi.
(PICHA NA ANNA NKINDA WA MAELEZO
)



  

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa amembeba mtoto Anna Julia Telles  mwenye umri wa miezi mitatu anayepata matibabu ya kansa katika Hospitali ya watoto wanaougua ugonjwa huo iliyopo mjini Brasilia nchini Brazili. Hospitali hiyo inatoa dawa aina ya chemotherapy kwa wagonjwa ambao ni watoto 500 kwa mwezi  na inatibu asilimia sabini ya kansa.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimtazama mtoto anayepata matibabu ya kansa katika Hospitali ya watoto wanaougua ugonjwa huo iliyopo mjini Brasilia nchini Brazili. Hospitali hiyo ambayo inapokea wagonjwa 4000 kwa mwezi  inatibu asilimia sabini ya kansa na hivyo kuwawezesha wagonjwa ambao ni watoto  kuendelea kuishi.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiangalia moja ya bidhaa zinazouzwa na Hospitali ya watoto wanaougua ugonjwa wa kansa kwa ajili ya kupata fedha za kuwasaidia watoto hao huku Afisa ubalozi wa Tanzania nchini Brazili Tabu Makata akimuangalia.  Hospitali hiyo iliyopo mjini Brasilia nchini Brazili inatoa  dawa aina ya chemotherapy kwa wagonjwa ambao ni watoto 500 kwa mwezi  na inatibu asilimia sabini ya kansa.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimsikiliza mfanyakazi wa Hospitali ya watoto waougua ugonjwa wa kansa akielezea jinsi hospitali hiyo pamoja na jamii inavyotoa huduma ya kujitolea kwa wagonjwa. Hospitali hiyo iliyopo mjini Brasilia nchini Brazili inatoa  dawa aina ya chemotherapy kwa wagonjwa ambao ni watoto 500 kwa mwezi  na inatibu asilimia sabini ya kansa.

No comments: