Mkwaju wa mbali wa Arteta umeipa ushindi Arsenal
Mkwaju wa mbali wa Mikel Arteta umeipa Arsenal ushindi muhimu na kuiacha Manchester City ikiwa pointi nane nyuma ya Manchester United katika ligi kuu ya England.
Mara mbili Robin Van Persie aligonga mwamba huku mkwaju mwingine aliopachika wavuni ukiwa wa kuotea.
Mashabiki wa Arsenal wakishangilia
Arsenal walitawala kabisa Mechi hii na kukosa bao mbili za wazi na Man City walikuwa na wakati mbovu hasa yule ‘Toto Tundu’-‘Kwanini kila Siku mie’- Mario Balotelli akistahili kupewa Kadi Nyekundu mara 3 katika Kipindi cha Kwanza lakini akaambulia Kadi ya Njano na hatimaye kupata nyingine ya pili katika Dakika ya 89 na kutolewa kwa Kadi Nyekundu. 
Bao la ushindi kwa Arsenal, bao tamu sana, lilifungwa Dakika ya 86 na Mikel Arteta kwa kigongo cha mbali.
Vikosi vilivyoanza:
Arsenal: Szczesny, Sagna, Koscielny, Vermaelen, Gibbs, Arteta, Song, Walcott, Rosicky, Benayoun, van Persie
Akiba: Fabianski, Andre Santos, Oxlade-Chamberlain, Ramsey, Djourou, Jenkinson, Chamakh.
Man City: Hart, Zabaleta, Kompany, Lescott, Clichy, Toure Yaya, Barry, Milner, Aguero, Nasri, Balotelli
Akiba: Pantilimon, Richards, Pizarro, Dzeko, Kolarov, Tevez, De Jong.
Refa: Martin Atkinson
Arsenal sasa wamerejea katika nafasi ya tatu, pointi mbili juu ya Tottenham walio nafasi ya nne.
Nimekuvumilia sana toka nje sasa.... Mario Balotelli akipewa kadi nyekundu
Mwisho: Dakika 90 zikaisha Man city wakatoka kapa na huku wakiduwaa kama ligi imeisha.
[MECHI ZILIZOBAKI kwa Man United & Man City]
Man City | Man Utd |
Jumatano Aprili 11 Man City v West Brom Jumamosi Aprili 14 Norwich v Man City Jumapili Aprili 22 Wolves v Man City Jumatatu Aprili 30 Man City v Man Utd Jumamosi Mei 5 Newcastle v Man City Jumapili Mei 13 Man City v QPR | Jumatano Aprili 11 Wigan v Man United Jumapili Aprili 15 Man United v Aston Villa Jumapili Aprili 22 Man United v Everton Jumatatu Aprili 30 Man City v Man United Jumamosi Mei 5 Man United v Swansea Jumapili Mei 13 Sunderland v Man United |
Arsenal nao ushindi kwao ni muhimu kujihakikishia wanashiriki UEFA mwaka huu.
Nani unadhani atashinda mchezo huu.? Maoni yako.
Timu | Michezo | GD | Pointi | ||||
---|---|---|---|---|---|---|---|
| 31 | 49 | 76 | ||||
Man City | 31 | 50 | 71 | ||||
| 32 | 20 | 59 | ||||
Arsenal | 31 | 21 | 58 | ||||
Chelsea | 31 | 18 | 56 | ||||
Newcastle | 32 | 6 | 56 |
No comments:
Post a Comment