Tuesday, April 24, 2012

MY TANZANIA

Picha hizi zilipigwa tukiwa njiani kurudi campsite baada ya kumaliza mizunguko (game drive) ndani ya pori la akiba la Selous. Ukiwa unatoka kuelekea Kijijini (Mloka) utapita mahali ambapo ndio mpaka wa game reserve na eneo la kijiji.

Hii sio njia inayotumiwa na wageni bali ni njia ambayo inatumiwa na wahifadhi kufanya ukaguzi wa mipaka ya hifadhi. Kimsingi, barabara hii ni sehemu/alama ya mpaka wa pori la akiba. Upande wa kulia wa Barabara ni Pori la Akiba wakati upande wa kushoto wa barabara ni eneo la Kijiji cha Mloka.

Huu ni barabara iliyo upande mwingine

Kibao kinachotoa mwongozo kwa mgeni anayeingia Selous GR


Shadowing the seasonal movements of the Serengeti wildebeest migration, this camp is a simple blend of form and function. Superlative game viewing from an oasis of safari civilization.


J


Picha nimeipiga nikiwa navuka mpaka toka Tanzania kuingia kwa watani wa Jadi. Milima unayoiona na Majengo vipi kwao (+254).

Arusha mpaka Namanga

Wiki iliyopita nilikuwa njiani kuelekea kwa watani zetu wa jadi kupitia mpaka wa Namanga. Mtundiko huu una baadhi ya taswira nilizoweza kuzinasa nikiwa njiani. Zote ni za maeneo kuanzia nje kidogo ya jiji la Arusha kuelekea Namanga.
Hapa ni maeneo ya Longido njiani kuelekea Namanga

Kwa wazoefu wa barabara ya Arusha Namanga watakuwa wanaijua vyema hii Savanah. ni Sehemu ambayo mandhari yake inashabihiana na hifadhi ya taifa ya Serengeti - ule uwanda wa nyasi.


hali ya barabara kati ya Arusha mpaka Namanga ni nzuri na lami imekamilika. japo sehemu chache ndio kuna marekebisho madogo madogo ya culverts ambazo zitamlazimu dereva kutumia njia ya pembeni. licha ya hivyo, diversion nazo zimeandaliwa vyema.

No comments: