Tuesday, April 10, 2012

VIONGOZI WA SIASA WAOMBOLEZA KIFO CHA STEVEN KANUMBA LEADERS

MAKAMU WA RAIS DK. GHARIB BILAL AONGOZA KUAGA MWILI WA STEVEN KANUMBA LEADERS, JIJI LA DAR ES SALAAM LAZIZIMA KWA SIMANZI

 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. Gharib Bilal akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa marehemu Steven Kanumba ulioagwa leo kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam huku viongozi mbalimbali wa Serikali, viongozi wa dini, Wanasiasa, Wanamuziki Waigizaji na watu maarufu wamejitokeza kuuaga mwili wa mwigizaji huo aliyekuwa maarufu zaidi nchini Tanzania na nje ya nje ya nchi pia, Marehemu Steven Kanumba anazikwa mchana huu kwenye makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam fourwaysbukoba.b inamuvuzisha matukio haya kutoka mjini Dodoma kupitia Sitlite zake zilizotegwa katika viwanja vya Leaders na Makaburi ya Kinondoni kwa matukio zaidi anedelea kufuatilia mtandao wako wa jamii kuhusu tukio hilo kubwa na la kushtua nchini mwetu kwa kumpoteza manafilamu mahili Steven Kanumba logspot.com
 
 
Picha ya chini wa pili kutoka kushoto  ni Mama wa Marehemu Steven Kanumba Bi. Flora Mgoa akiwa katika hali ya majonzi mwisho kushoto ni Mkurugenzi wa ASET Asha Baraka akimfariji Mama Kanumba
 



Mmoja wa waombolezaji akisidiwa na wafanyakazi wa msalaba mwekundu mara baada ya kuzimia katika msiba huo mkubwa.
Kutoka kulia ni Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi, Ridhiwan Kikwete, Mbunge wa Jimbo la Kinondoni Idd Azzan na waombolezaji wengine wakiwa katika msiba huo.
Kundi maalum lililoandaliwa kwa nyimbo za maombolezo likiimba nyimbo za maombolezo katika katika msiba huo.
Jeneza la mwili wa marehemu Kanumba likiwa limewekwa tayari kwa waombolezaji kutoa heshima zao za mwisho
Ndugu  wa karibu wakielekea sehemu waliyotengewa kukaa.
Askari wa kike wakiweka sawa utaratibu wa waombolezaji kupita katika eneo hilo ili kukaa.
Rais wa Shirikisho la wasanii wa Filamu Saimon Mwakifwamba akizungumza katika msiba huo kutoa salamu zao za rambirambi kwa marehemu Steven Kanumba
Mmoja wa waombolezaji akipitishwa juu juu kwenye vichwa vya waombolezaji ili kupata huduma ya kwanza baada ya kuzirai, katikati anayetazama mbele ni Mussa Kisoky Mkurugenzi wa kampuni ya Sofia Production ya jijini Dar es salaam.
Mwigizaji Steven Jacob kushoto akizungumza  jambo na mbunge wa Maswa Mashariki Mh. John Shibuda katikati.
Mr Mtitu kulia akijadili jambo na mmoja wa waombolezaji wa
Utaratibu unapangwa na wanakamati wa kamati ya mazishi
Gari lililobeba mwili wa marehemu Kanumba linaondoka Leaders kwenda Makaburi ya Kinondoni huku likiwa limezungukwa na waombolezaji.
Umati wa waombolezaji ukiondoka kuelekea makaburi ya Kinondoni.
Jeneza lenye Mwili wa Marehemu,Steven Kanumba likiwasili kwenye Viwanja vya Leaders Club,jijini Dar es Salaam asubuhi hii.  Makamu wa Rais,Dkt. Mohamed Gharib Bilal akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Steven Kanumba asubuhi hii kwenye viwanja vya Leaders Club,Jijini Dar es Salaam.akifuatiwa na Mkewe,Pamoja na Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete (mwenye nguo nyeupe kulia). Mh. Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu akitoa heshima za mwisho.
Kwaya maalum ikiimba nyimbo za maombolezao katika msimba huo kwenye viwanja vya Leaders
Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi akipiga sal;ute mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu Steven Kanumba kama ishara ya kumkubali kwake na kutoa heshima kwa marehemu Steven Kanumba.


Mama mzazi wa Kanumba akiwapungia mkono mashabiki wa mwanae waliokuwa viwanja vya leaders wakiuaga mwili wa marehem

watoto wawili walikuwa aki act na marehem Kanumba wakiingia viwanjani

Mwili wa marehemu ukifikishwa viwanjani tayari kwa kumpa heshima ya mwisho




picha zote na dj choka
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. Gharib Bilal akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa marehemu Steven Kanumba ulioagwa leo kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam huku viongozi mbalimbali wa Serikali, viongozi wa dini, Wanasiasa, Wanamuziki Waigizaji na watu maarufu wamejitokeza kuuaga mwili wa mwigizaji huo aliyekuwa maarufu zaidi nchini Tanzania na njeya nje ya nchi pia, Marehemu Steven Kanumba anazikwa mchana huu kwenye makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam

Jeneza lenye Mwili wa Marehemu,Steven Kanumba likiwasili kwenye Viwanja vya Leaders Club,jijini Dar es Salaam asubuhi hii.  Makamu wa Rais,Dkt. Mohamed Gharib Bilal akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Steven Kanumba asubuhi hii kwenye viwanja vya Leaders Club,Jijini Dar es Salaam.akifuatiwa na Mkewe,Pamoja na Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete (mwenye nguo nyeupe kulia). Mh. Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu akitoa heshima za mwisho.
Kwaya maalum ikiimba nyimbo za maombolezao katika msimba huo kwenye viwanja vya Leaders
Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi akipiga sal;ute mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu Steven Kanumba kama ishara ya kumkubali kwake na kutoa heshima kwa marehemu Steven Kanumba.

 Waigizaji wenzake na marehemu Steven Kanumba kutoka kulia ni  Mr. Mtitu na Raymond Kigosi wakiwa katika jukwaa kuu mahali ambapo mwili wa marehemu umewekwa kwa ajili ya waombolezaji  kuuaga kwa mara ya mwisho
 Mbunge wa Mbeya Mjini na msanii  wa muziki wa HipHop Joseph Mbilinyi aka Mr Sugu akihojiwa na waandishi wa habari katika msiba huo.
Katibu wa CCM Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na vyombo vya habari katika msiba huo mkubwa na ulioitikisa nchi.

STEVEN KANUMBA KWELI ALIKUWA MTU WA WATU, MAELFU WAKO LEADERS KUMUAGA MCHANA HUU

Mwigizaji Clouds pamoja na waombolezaji wengine wakiwa wamebeba jeneza la mwili wa Mwigizaji mwenzao marehemu Steven Kanumba aliyefariki hivi karibuni kwa ajili ya kuuweka mahali palipoandaliwa kwa ajili ya waombolezaji kuuaga mwili wa mpedwa wao katika viwanja vya Leadres jijini dar es salaam, Marehemu Kanumba ataagwa leo hapo na kuzikwa katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam.
Fullshangweblog  inarusha matukio haya kutoka mjini Dodoma kupitia sitelite zilizotegwa kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam
(PICHA NA MP)



Mwili wa marehemu Kanumba ukiwa umewekwa tayari kw awaombolezaji kuuaga kwa mara ya mwisho.
Waombolezaji wakiwa wamefurika kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam kwa ajili ya kuuaga mwili wa Marehemu Kanumba.
Wafanyakazi wa Msalaba Mwekundu wakiwa wamembeba mmoja wa waombolezaji aliyepoteza fahamu kwa ajili ya majozi ya msiba huo.
Wafanyakazi wa msalaba mwekundu wakiwa tayari kwa kuwahudumia watu watakaopata matatizo yoyote kutokana na msiba huo.
Mmoja wa waombolezaji akiwa anasaidiwa na mwenzake
Usalama umeimarishwa katika viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam kwa ajili ya msiba huo.
Kama unavyoona katika picha usalama ni mkubwa na watu wameandaliwa maeneo ya kukaa kwa ajili ya msiba huo.
Waombolezaji mbalimbali wakiingia katika viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam.
Ni hali ya majonzi pamoja na kwamba kuna jua kali lakini waombolezaji wengi wamejitokeza katika viwanja hivi.
Makapeti mekundu yametandikwa katika viwanja hivyo kwa ajili ya kupita viongozi na watu maarufu.

Daktari aeleza kilichomwua mwigizaji Steven Kanumba

Habari hii kwa hisani ya www.mwananchi.co.tz/ 
Florence Majani na Suzzy Butondo

MSANII nyota wa filamu nchini, Steven Kanumba amefariki dunia kutokana na tatizo la mtikisiko wa ubongo linalojulikana kitalaamu kama Brain Concussion, taarifa za kitabibu zimeeleza.
Taarifa hizo za ndani, zilizopatikana jana baada ya jopo la madaktari bingwa watano wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kuufanyia uchunguzi mwili wa marehemu huyo, zimeeleza kuwa tatizo hilo linaweza kumfanya mtu apoteze maisha mara moja au baada ya siku kadhaa. Mmoja wa madaktari hao ambaye aliomba jina lake lisitajwe gazetini alisema waligundua tatizo hilo baada ya kumfanyia uchunguzi huo kwa zaidi ya saa mbili.

“Tulianza kuufanyia uchunguzi mwili wa marehemu kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi saa 6:45 mchana na tukagundua kuwa marehemu alifariki kutokana na mtikisiko wa ubongo kwa kitaalamu, Brain Concussion,” alisema daktari huyo. Alisema Kanumba alipata mtikisiko wa ubongo ambao husababisha kufeli kwa mfumo wa upumuaji (cardio-respiratory failure) “Kilichomuua hasa ni mtikisiko wa ubongo, ambao endapo unatokea katika sehemu ya nyuma ya ubongo (cerebrum), huua kwa haraka” alisema daktari huyo na kuongeza kuwa mtikisiko wa ubongo  wa nyuma, husababisha matatizo ya mfumo wa upumuaji na hilo limeonekana katika mwili wake.

“Baada ya ubongo wake kutikiswa kwa nguvu, mfumo wa upumuaji ulifeli na ndiyo maana tumekuta kucha za Kanumba zikiwa na rangi ya bluu, huku mapafu yake yakiwa yamevilia damu na kubadilika kuwa kama maini, hizo ndizo dalili za kufeli kwa mfumo wa upumuaji.”

“Mtu aliyepata mtikisiko wa ubongo huweza kutokwa na mapovu mdomoni na hukoroma kabla ya kukata roho na ndivyo ilivyokuwa kwa Kanumba kabla hajafariki.”

Daktari mwingine aliyeshiriki katika uchunguzi huo ambaye pia aliomba jina lake lisitajwe alisema ubongo wa mwigizaji huyo ulikuwa umevimba na kushuka karibu na uti wa mgongo na hivyo kuathiri mfumo wa upumuaji.
Alisema sehemu ya maini na majimaji ya machoni ya marehemu, vimepelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali ili kubaini endapo kuna sumu au kitu kingine katika mwili huo.

Baba mzazi azungumza Baba mzazi wa mwigizaji huyo, Charles Musekwa Kanumba alisema kwamba alipata taarifa za kifo cha mwanawe Jumamosi saa 10:00 alfajiri baada ya kupigiwa simu na dada wa marehemu, Sara Kanumba.  “Sara aliniuliza: ‘Una taarifa yoyote kuhusu mwanao Kanumba?’ Nikamjibu kuwa sina taarifa yoyote, ndipo aliponieleza habari za kifo hicho. Aliniambia Kanumba hatupo naye tena amefariki kwa kuanguka, amekorofishana na mpenzi wake.”  alisema taarifa hizo zilimsababisha aishiwe nguvu kwa kuwa kilikuwa kifo cha ghafla… “Basi kuanzia hapo, nilianza kupigiwa simu za kupewa pole, ndipo nilipoamini kumbe mwanangu amefariki.”

 Akizungumzia kuchelewa kufika msibani, alisema kumetokana na tatizo la mawasiliano. Awali, alikuwa amepanga mtoto wake Kanumba akazikiwe Mwanza kwa babu yake ndiyo maana hakufika mapema msibani.   “Nilikuwa nimepanga apitishwe hapa kwangu Shinyanga aagwe, halafu tumpeleke Mwanza kwa babu yake kumzika huko lakini alipokuja mama yake alinishauri kuwa huko kutakuwa na nafasi ndogo kwa sababu watu ni wengi pia alikuwa na marafiki wengi, wengine wa kutoka nje ya nchi kwa hiyo alinishawishi na tukakubaliana kumzika Dar es Salaam,” alisema.

No comments: