' Madudu Ya Ekelege'- Waziri Chami Amwandikia Rais Kumshauri Amwajibishe
Hatua hiyo ya Dk Chami imekuja baada ya wabunge kuchachamaa bungeni wakitaka Waziri Chami ajiuzulu kwa kile kinachodaiwa kumkingia kifua mkurugenzi huyo.
Licha ya shinikizo hilo, Waziri Chami alikuwa akijitetea kuwa asingeweza kumchukulia hatua mkurugenzi huyo bila kuwa na tuhuma ambazo zingempa nguvu ya kumshauri Rais.
Dk Chami alikuwa akisema kuwa hadi bunge linamalizika mjini Dodoma wiki hii alikuwa hajaiona ripoti ya Kamati Ndogo ya Bunge iliyomchunguza Ekelege ambayo ingemsaidia kupata tuhuma zinazomkabili.
“Hata ripoti maalumu ya ukaguzi iliyofanywa na CAG mpaka wabunge wanapaza sauti pale bungeni sikuwa nimeiona na Ekelege ni mteule wa Rais nitamwambia Rais amefanya nini?”
Mkurugenzi huyo mkuu anatuhumiwa kuisababishia Serikali hasara ya Sh18 bilioni kutokana na utendaji mbovu katika kusimamia ukaguzi wa magari yanayoingia nchini uliokuwa ukifanywa na mawakala nje ya nchi.
Dk Chami alithibitisha jana kuwa baada ya kupokea taarifa ya CAG Aprili 18, mwaka huu siku iliyofuata alimwandikia barua Rais akimuomba amsimamishwe kazi Ekelege.
Alisema amemuomba Rais afanye mambo mawili, kumpa likizo ya malipo ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili na pia airuhusu Bodi ya Wakurugenzi kuteua kaimu katibu wake." ( Mwananchi, Aprili 28, 2012)
No comments:
Post a Comment