Tuesday, April 10, 2012

YALIYOJIRI KATIKA VIWANJA VYA LEADERS WAKATI WA KUAGA MWILI WA MAREHEMU STEVEN KANUMBA LEO


 Fullshangweblog.com inakuletea matukio kadhaa yaliyojiri katika viwanja vya Leaders wakati wa tukio kubwa la kuuaga mwili wa Mwigizaji marehemu Steven Kanumba kama picha hii ya kwanza inavyoonyesha Makamu wa Rais akimfariji mama mzazi wa marehemu Steven Kanumba Bi. Flora Mgoa, wakati alipokwenda kutoa heshima zake za mwisho kwa marehemu mwigizaji huyo aliyefanya vizuri sana katika tasnia ya filamu nchini Tanzania na nje ya Tanzania.
 Waigizaji mbalimbali wakiwa katika msiba huo kwenye viwanja vya Leaders leo.
 Rais wa shirikisho la filamu Nchini Bw. Saimon Mwakifwamba akimfariji mmoja wa waombolezaji katika msiba huo.
 Mmoja wa waombolezaji akibebwa juu juu baada ya kuzirai katikamsiba huo.
 Huyu naye hakujiweza ilibidi asaidiwe na wafanyakazi wa Msalaba mwekundu.
 Huyu muombolezaji naye alidondoka baada ya kupoteza fahamu na kuzirai katika viwanja vya Leaders.
 Watoto waliowahi kuigiza na marehemu Steven Kanumba na ambao aliibua vipaji vyao yeye mwenyewe wakiwa wamebea picha ya Marehemu Kanumba.
 Hali ilikuwa ni ya majonzi na waombolezaji wengi walidondoka chini na kupoteza fahamu kutokana na simanzi.
 Viongozi mbalimbali wamehudhuria katika kutoa heshima zao za mwisho kwa marehemu kutoka kulia ni Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Meck Sadik, Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernald Membe, Waziri wa Ardhi na Makazi Prof. Anna Tibaijuka na Mbunge wa jimbo la Kinondoni Mh. Idd Azzan.
Mtangazaji wa Clods TV Regina Mwalekwa akiwajibika katika tukio hilo la kihistoria kwenye viwanja vya Leaders.

No comments: