Wednesday, May 30, 2012

Hatimaye Mtuhumiwa John Warburg atiwa nguvuni na Polisi baada ya Kuruka Dhamana Kituo Cha Urafiki



Kachero kutoka Polisi Arusha, D/CPL Fortunatus (mwenye tisheti ya pundamilia kushoto), akiimarisha ulinzi wakati Mtuhumiwa wa Kesi ya Wizi wa Kuaminiwa, Bw. John Warburg (mwenye tisheti nyekundu), akiteremka kutoka kwenye Basi la Ngorika katika Kituo cha Mabasi cha Ubungo jijini Dar es Salaam leo Mei 29.2012, wakitokea jijini Arusha ambako Mtuhumiwa Warburg alikamatwa kufuatia kuruka dhamana aliyopatiwa katika Kituo cha Polisi cha Urafiki takribani Miezi Mitatu iliyopita. John Warburg alidhaminiwa katika Kituo cha Polisi Urafiki baada ya kukamatwa akituhumiwa kwa kosa la kujipatia Gari aina ya Toyota Cresta GX 100 lenye namba za usajili T 796 AVQ na kuliuza kwa manufaa yake bila idhini ya mwenye mali kesi yenye kumbukumbu namba URP/RB/2412/2012 -.URP/IR/1544/2012. PICHA/DAILY MITIKASI BLOG


Mdhamini wa Mtuhumiwa John Warburg Bwana Max Kafipa (kulia), akiwa bega kwa bega na mtuhumiwa wake kuhakikisha anafika Kituo cha Polisi Urafiki.Kushoto ni D/CPL Fortunatus wa Polisi Arusha, aliyemu-escort mtuhumiwa hadi hapa jijini.

No comments: