Saturday, May 26, 2012

TANZANIA BEGA KWA BEGA NA UNDP KUJENGA AFRIKA YENYE UHAKIKA WA CHAKULA.

Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa UNDP nchini Tanzania Dk. Alberic Kacou akizungumza kwa niaba ya UNDP kuhusiana na kuzinduliwa kwa Ripoti ya Maendeleo ya Afrika 2012 ambapo amesema huu sasa ni wakati kwa nchi za Afrika haswa zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara kujenga mazingira ya kuelekea mustakabali wenye uhakika wa chakulaPicha na MO BLOG

Mgeni rasmi Mh. Janet Mbene na Dk. Alberic Kacou wakionyesha Ripoti hiyo kwa wageni waalikwa na waandishi wa habari mara baada ya kuizindua rasmi leo.

Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Fedha Mh. Janet Mbene na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Tanzania, Dk. Alberic Kacou (kulia) wakifuatilia maoni ya Uchambuzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Afrika 2012 kutoka kwa Maprofesa wa Vyuo vikuu nchini.
Baadhi ya Wageni waalikwa wakipitia Ripoti ya Maendeleo ya Afrika 2012 kuelekea kwenye Mustakabali wenye uhakika wa Chakula kwa nchi za Afrika iliyozinduliwa rasmi leo jijini Dar es Salaam.

Na.Mwandishi wetu.

Bara la Afrika ikiwemo Tanzania limeshakumbwa na matukio kadhaa ya kukabiliwa na uhaba wa chakula, uliokwenda sambamba na matukio ya watu wengi kupoteza maisha haswa Kusini mwa jangwa la Sahara na Ukanda wa Sahel eneo la Afrika Magharibi.

Hali hiyo imekuwa moja ya changamoto kubwa inazozikabili serikali za mataifa hayo ambapo yanapambana ili kuitatua ili kila mwananchi barani Afrika aweze kufurahia kukua kwa uchumi.

Akitoa hotuba wakati akizindua rasmi Ripoti ya Maendeleo ya Afrika 2012 leo jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Fedha Mh. Janet Membe (MB) amesema kwa muda mrefu sura ya eneo la nchi za Afrika zilizo Kusini mwa jangwa la Sahara imekuwa ni ya njaa ya kukithiri, ambapo zaidi ya mtu mmoja katika kila waafrika wane wana tatizo la upungufu wa lishe.

Amesema Ripoti hiyo inaonyesha kuwa pamoja na ukweli kwamba baadhi ya nchi zinazokuwa kwa kasi kiuchumi katika kipindi cha miaka kumi ziko Afrika, lakini bado hali ya maisha ya waafrika ni duni.

Awali Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa UNDP nchini Tanzania Dk. Alberic Kacou alisema bara la Afrika limejaliwa kuwa na ardhi yenye rutuba, maji ya kutosha na hali nzuri ya hewa kwa kukuzia mazao, lakini swali la kujiuliza ni kwanini bado kuna uhaba wa chakula.

Hata hivyo Dk. Kacou ametoa matumaini kuwa bara la Afrika bado lina uwezo wa kujijengea mazingira ya kuwa na akiba ya kutosha ya chakula kwa kipindi kijacho.

Ripoti hii ya Kwanza ya Maendeleo ya Afrika inasema kwamba ongezeko endelevu katika uzalishaji kwenye kilimo kunalinda haki ya chakula na uwezo wa watu kupata chakula.

No comments: