Tuesday, May 8, 2012

JITIHADA MADHUBUTI ZA KUPUNGUZA UMASIKINI ZINAPASWA KULENGA UCHUMI WA WAKAZI WA VIJIJINI

NA PALINE KUYE -IRINGA
 
Jitihada madhubuti za kupunguza umasikini na kuleta maendeleo, zinapaswa kulenga wakazi na uchumi wa vijijini, ili kuwa na matokeo mazuri ya maendeleo nchini .
 
Hayo yamesemwa na makamu wa Rais Mohamed Gharib bilal, katika uzinduzi wa jukwaa la uchumi wa kijani, ambalo limeanzishwa na taasisi ya uongozi uliofanyika katika ukumbi wa mtakatifu dominic uliopo katika manispaa ya Iringa.
 
Amesema kuwa jukwaa la uchumi wa kijani linalenga kuongeza uelewa wa watunga sera,watoa maamuzi, na wananchi wenyewe ushawishi mkubwa katika jamii kuhusu umuhimu wa kuzingatia matumizi endelevu ya rasilimali, katika shughuli za kukuza uchumi.
 
 
Bilal amesema kuwa katika maeneo mengi ya vijijini mazingira yameendelea kuingiliwa na matumizi shindani ya rasilimali kwa maslahi ya kibiashara, ambayo yamesababisha hasara katika jamii ikiwa ni pamoja na upotevu wa maisha na kipato.
 
Aidha mpango huo utatoa fursa kwa makundi mbalimbali ya kijamii kukutana na kubadilishana mawazo na kufanya kazi pamoja ili kuongeza kasi ya maendeleo ya kijani nchini Tanzania, pamoja na kujenga mtaji wa kijamii kwa ajili ya uchumi wa kijani nchini.

No comments: